Kama ni mtumiaji wa Instagram Tanzania inabidi uyajue haya mabadiliko
Walisema Tanzania inaongoza Afrika kwa kuwa na watumiaji
wengi wa mtandao wa kijamii wa Instagram na ndio maana naamini mabadiliko
yaliyotokea yanatakiwa kuwafikia Watanzania.
Kama
hujagundua kwenye page yako ya Instagram ni kwamba kila unapopost video ya
sekunde 15 kama ulivyo utaratibu wa kawaida wa Insta, mabadiliko mapya
yaliyofanywa na mamlaka ya mtandao huu wa kijamii ni kukupa fursa wewe na
followers wako kuonavideo
uliyopost imetazamwa na watu wangapi kama inavyoonekana hapa chini.
Kwenye mabadiliko haya
ya Instagram, mtandao wa kijamii wenye watumiaji zaidi ya milioni 400, likes
hazitoonekana mpaka ubonyeze sehemu yenye idadi ya views ndio itakupeleka kuona
likes za hiyo post.
pango huu mpya wa Instagram ulitangazwa
zaidi ya siku kumi zilizopita na mabadiliko nimeanza kuyaona Tanzania
kuanzia February 22 2016.
No comments: