Seth Bosco.ajutia kuponzwa na starehe
Stori: brighton masalu
Mdogo wa aliyekuwa nguli wa filamu Bongo, Steven Kanumba, Seth Kamugisha Bosco amekiri kujisahau na kuponzwa na starehe kwa kushindwa kufuata misingi na maagizo ya kaka yake na kwamba kwa sasa amerejea ‘mstarini’ kwa kufuata yote aliyohusiwa.
Akizungumza na mwandishi wetu kwa njia ya simu hivi karibuni, Seth alisema starehe na ukaribu wake na wanawake vilimfanya ajisahau na kwamba kwa sasa ameamua kuyafanyia kazi yale yote ambayo alijifunza kutoka kwa Kanumba.
“Unajua ujana una mambo mengi sana, kujisahau na kubweteka, starehe za pombe na wanawake zimekuwa zikituponza sana, nilijisahau lakini kwa sasa nimezinduka na hivi ninavyoongea na wewe nakamilisha kazi moja ambayo kwa kweli itarejesha heshima yangu,” alisema Seth
No comments: