Mrembo ateswa uarabuni
MATESO! Ndivyo unavyoweza kusema kufuatia mrembo Sada Hussein, mkazi wa Tandale kwa Mtogole jijini Dar kupata mateso mazito baada ya kupelekwa Uarabuni nchini Oman kwa lengo la kufanya kazi za ndani, tofauti na matarajio, alijikuta akiteswa vibaya na muajiri wake.
Akizungumzia tukio hilo kwa uchungu, kaka wa msichana huyo aliyejitambulisha kwa jina la Mashaka, alisema walikuwa wakiishi na ndugu yao huyo nyumbani kwao Tandale kwa Mtogole ndipo alipotokea kijana mmoja ambaye ni jirani yao na kumwambia kuna nafasi ya kazi za ndani nchini Oman hivyo kama wako tayari, awaunganishe kwa mama mmoja aliyefahamika kwa jina la Zamda Seleman ambaye ndiyo dalali.
“Nilipewa taarifa na jamaa ambaye ni wa mtaani kwetu nikaona hii nafasi ngoja nimuunganishie mdogo wangu kwa kuwa hana kazi na akifanikiwa atusaidie na sisi maana hali yetu kiuchumi si nzuri,” alisema Mashaka.
Akiendelea kusimulia, Mashaka alisema baada ya kuzungumza na mdogo wake huyo na kukubali, walimuita mama huyo dalali ambapo walizungumza naye, wakakubaliana malipo ya shilingi laki mbili na nusu kila mwezi, akamsafirisha Sada kwa gharama zake kwenda nchini Oman.
Akiendelea kusimulia, Mashaka alisema baada ya kuzungumza na mdogo wake huyo na kukubali, walimuita mama huyo dalali ambapo walizungumza naye, wakakubaliana malipo ya shilingi laki mbili na nusu kila mwezi, akamsafirisha Sada kwa gharama zake kwenda nchini Oman.
Mashaka alisema baada ya miezi kadhaa kupita, alipata taarifa kutoka kwa wasichana wawili waliotokea nchini Oman kuwa Sada ananyanyaswa na mwajiri wake alipokuwa akidai mshahara alikuwa akipigwa sana mwisho akamtelekeza katika ubalozi wa Tanzania nchini Oman.
“Nilioneshwa picha na wadada wawili ambao Sada aliwaelekeza namna ya kufika nyumbani kwa kuwachorea ramani, wakafika ndipo tukaanza kufuatilia. Tulianzia kituo cha polisi Magomeni, tukapewa RB/MAG/PE/208/15 kisha tukaenda ubalozi wa Oman nchini, tukasaidiwa, Sada akarejeshwa nchini,” alisema Mashaka.
Akiendelea kusimulia, Mashaka alisema baada ya kufungua taarifa polisi, Zamda alikamatwa na baada ya siku moja aliachiwa kisha kukiuka masharti ya kulipia gharama za matibabu ambazo walimtaka amlipe mgonjwa wao kutoka kwenye mishahara ya miezi minne aliyofanya kazi bila kulipwa lakini yeye akawapa mshahara wa mwezi mmoja pekee (laki mbili na nusu).
“Huwezi amini, tulipokabidhiwa ndugu yetu pale Polisi Magomeni, machozi yalitutoka kwani ndugu yetu hazungumzi wala hatusikii tunamuongelesha zaidi ya kutabasamu tu mbaya zaidi huyo mama naye akaleta jeuri, akakataa kutulipa fedha zote za mshahara alizokuwa anadai ndugu yetu,” alisema Mashaka.
Akizungumza Sada mwenyewe kwa njia ya ishara nyumbani kwao, alisema alikuwa akipata kipigo tangu alipoanza kudai mshahara wa kwanza na kulala kwake ilikuwa saa sita usiku na kuamka saa kumi alfajiri kutokana na wingi wa kazi.Alisema siku hiyo ya mwisho, walimpiga na kumbeba usiku wa manane na kwenda kumtupa nje ya ofisi ya ubalozi wa Tanzania ambapo alipata hifadhi hadi aliporudishwa nyumbani.
Baada ya kuzungumza na kaka wa Sada, gazeti hili lilimpigia simu mama ambaye alimpeleka Sada, Oman na aliposomewa shitaka lake alijibu kwa ujeuri kuwa yeye si msemaji kama ni taarifa zipo polisi.
“Siwezi kuzungumza chochote na wala siyo msemaji mkuu kama mnataka habari zaidi nendeni polisi,” alisema mama huyo
“Siwezi kuzungumza chochote na wala siyo msemaji mkuu kama mnataka habari zaidi nendeni polisi,” alisema mama huyo
No comments: