AUNTY EZEKIEL amkingia kifua IYOBO

Msanii wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel akiwa na mzazi mwenzake Moze Iyobo.
Stori: brighton masalu
KUFUATIA kuwepo kwa madai na minong’ono mingi ya msanii wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel kumzidi umri mzazi mwenzake, Moses Iyobo, muigizaji huyo ‘amewaka’ na kuwataka watu wasiingilie uhusiano wao na kwamba suala la umri kwao ni namba tu.
‘Akibananishwa ukutani’ na mwandishi wetu kwa maswali magumu hivi karibuni, Aunt alisema amekuwa akiumizwa na maneno yanayoendelea juu ya kumzidi umri Iyobo, na kusema hayuko tayari kuona uhusiano huo ukivunjwa kwa maneno ya aliowaita “wakosa kazi”.
“Kwani wakati tunatongozana hatukujua kuwa tunazidiana umri? Mbona watu wanashindwa kufanya mambo ya msingi na kukalia majungu? Kwetu sisi suala la umri ni namba tu, labda nikuulize, ulishaona mtoto anambebesha mwanamke mimba? Maneno ya mimi kumzidi umri Iyobo yananiumiza sana kwa kweli, lakini nitaulinda uhusiano huu hadi mwisho,” alisema Aunt Ezekiel.

No comments:

Powered by Blogger.