Mrema: Chadema mbona mnanishambulia, tatizo ni uzee wangu?.


Mwenyekiti Taifa wa chama cha Tanzania Labour Party TLP,  na mgombea Ubunge jimbo la Vunjo Augustino Mrema, amelalamikia kuwa anafanyiwa siasa chafu na wapinzani wake.

Akizungumza na waandishi wa habari jimboni Vunjo, Mrema amepeleka lawama moja kwa moja kwa viongozi wa chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA, kwa kumchafua kwa matusi kwenye kampeni pamoja na kufanyiwa ubaguzi.

“Siwalaumu wanachama wa CHADEMA, viongozi wao ndio wenye fujo na mimi, sasa najiuliza tatizo ni nini ,uzee wangu? kama ndio hivyo wawaachie wananchi, kama kuumwa mbona tangu 1984 naugua kisukari, kwa nini wananitendea haya?”

Katika ‘line’ nyingine, Mzee Mrema amedai bado ana imani na wananchi wa vunjo watampigia kura ili awaongoze kwa mika mingine mitano

No comments:

Powered by Blogger.