Mama Diamond amkimbia Zari
KWELI maisha si popote! Msemo huu wenye kinyume na ule usemao maisha ni popote umedhihirika baada ya hivi karibuni mapaparazi wetu kutonywa kuwa, mama wa Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Sanura Kasim amekuwa akimkimbia mkaza mwanaye, Zarinah Hassan ‘mama Tiffah’ ndani na kwenda kukaa nje kutokana na Zari kujikita sana kwenye mitandao ya kijamii hivyo kutokuwa na mawasiliano.
Zarinah Hassan ‘mama Tiffah’.
“Mnajua mama Diamond hana neno. Anaweza kukaa na Zari wakaongea, tatizo Zari. Muda mwingi yupo kwenye Instagram, mara WhatsApp, ukiangalia mama yeye na mambo hayo si sana. Anajikuta yuko mwenyewe tu.
“Ndiyo maana inafika wakati inabidi mwanamke huyo atoke ndani na kwenda kushinda nje. Zari mara nyingi yeye yupo na simu kwenye eneo la bwawa la kuogelea,” kilisema chanzo.
Mama wa Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Sanura Kasim.
UZUNGU KWA SANA
Chanzo kiliendelea kueleza kuwa, maisha ya mama Diamond na Zari ndani ya mjengo huo ni ya watu wawili tofauti.
“Zari anapenda sana mambo ya uzunguni. Si unajua maisha yake ya kitajiri halafu amezoea sana Afrika Kusini, akienda Uganda kwao ni mara mojamoja.
Mama Tiffah akifanya yake.
“Sasa mama Diamond yeye kazoea maisha ya ‘uswahilini’. Kujiachia kwa sana. Akiamua leo anataka kula ugali na bamia, Zari anataka kukaangiza sana. mara asubuhi chai na tambi, wakati mama mkwe wake anataka chai na vitumbua au mihogo yenye kachumbari. Si unaona wasivyo kopu”
NI KWELI HAWAENDANI?
Kwa mujibu wa chanzo, mama Diamond na Zari hawaendani kwa maana ya kila mmoja anapenda kitu ambacho mwenzake hakipendi au hajakizoea kukifanya katika maisha yake. Hata nyie waandishi semeni, mama Diamond na Zari wanaendana wapi!
“Lakini si kwamba ni wagomvi, hapana! Wako vizuri sana ila maisha tu. Zari ni ‘mzungu’ mama Diamond ni ‘mswahili’ sasa wapi kwa wapi!” kilisema chanzo.
MAMA DIAMOND ANASWA
Mwanzoni mwa wiki hii, mapaparazi wetu walifunga safari hadi Madale jijini Dar nyumbani kwa Diamond ili kuona kama kweli mwanamke huyo humkimbia mkaza mwanaye huyo ambaye ana kichanga na kwenda kukaa nje muda mwingi.
NI KWELI
Katika hali ya kushangaza, mapaparazi wetu walimkuta mama huyo akiwa amekaa kwenye kibaraza cha nyumba ya jirani eneo ambalo lina akina dada wanachoma maandazi ya kuuza na wateja wanafika wakifuata mahitaji ya vitafunwa hivyo.
Mama Diamond alionekana hana wasiwasi na alikuwa akitumia muda mwingi kuzungumza na wakaanga maandazi hao.
APIGA STORI NA WAPITA NJIA
Mbali na kuzungumza muda mwingi na wakaanga maandazi, pia mama Diamond alikuwa akizungumza na wapita njia ambao walikuwa wakitoka sehemu moja kwenda nyingine.
MAJIRANI WAMCHAMBUA
Baadaye, mapaparazi wetu walipata nafasi ya kuzungumza na majirani wa mama Diamond ambapo wengi walimchambua vilivyo.
“Sisi hatukutegemea kama angekuwa ni mwanamke wa kuja kukaa nje na majirani zake. Mama Diamond ni wa ajabu sana. uwezo wa mwanaye, angekuwa mwanamke mwingine hata salamu tusingepata.
“Yeye amekuwa mtu wa watu. Akiwa na nafasi atatoka nje kama unavyomwona pale, anaongea baadaye anarudi ndani kwake,” alisema jirani mmoja mwanamke akikataa kutaja jina lake.
“Mimi sina la zaidi, ila nasema Mungu ambariki mama Diamond. Ni mwanamke asiyejionesha kwamba ana mtoto mwenye jina kubwa hapa Tanzania na Afrika kwa ujumla. Anajibeba yeye kama yeye. Sasa kama ndani anakimbia kukaa na mkewe Zari sisi hatujui,” alisema mwanamke mwingine.
MAMA DIAMOND
Alipofuatwa mama Diamond ili azungumzie madai ya kumkimbia Zari ndani, alikuwa ameshazama ndani ya geti na mlinzi alikuwa mkali kutoa ushirikiano.
Simu yake ya mkononi iliita bila kupokelewa huku ikielezwa kuwa, namba asizozijua ni mgumu wa kupokea simu
No comments: