YANGA HAIKAMATIKI

DSC_0253
Mabingwa wa ligi ya kuu ya Vodacom Tanzania bara Yanga wameendelea kushinda mechi zao za ligi licha
ya kutangaza ubingwa kabla ya mechi za ligi kumalizika.
Yanga wameichapa Mbeya City kwa bao 2-0 kwenye uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya na kuendelea kujikusanyia pointi za kutosha kunako VPL, Yanga imefikisha jumla ya pointi 71 baada ya kucheza michezo 28 huku ikiwa imesaliwa na michezo miwili kabla ya ligi kufika tamati.
Bao la kwanza la Yanga limefungwa na beki wa kati Vicent Bosou dakika ya 16 kipindi cha kwanza ambaye aliunganisha kwa kichwa krosi ya Juma Abdul aliyeanziwa mpira wa kona na Simon Msuva.
Tambwe aliifungia Yanga bao la pili dakika za lala salama kwa shuti kali akiwa nje ya box, bao hilo ni la tatu mfululizo kwake kwenye mechi za ligi lakini ni bao lake la 21 kwenye ligi akimuacha Hamisi Kiiza kwa magoli 2 nyuma.
DSC_0225
Mambo muhimu ya kufahamu.
  • Juma Kaseja na Ramadhani Chombo ‘Redondo’ ni wachezaji wa Mbeya City ambao wamecheza kwenye mchezo dhidi ya Yanga lakini waliwahi kukutana kwenye mechi za watani wa jadi kati ya Simba na Yanga misimu kadhaa kabla iliyopita.
  • Deus Kaseke na Juma Kaseja ni wachezaji wawili ambao leo wamecheza dhidi ya timu zao za zamani. Kaseke alikuwa akiitumikia Mbeya City kabla ya kujiunga na Yanga wakati Kaseja yeye alikuwa mchezaji wa Yanga kabla ya kuingia kwenye mgogoro na hatimaye kuhamia Mbeya City.
  • Kocha msaidizi wa Yanga Juma Mwamusi alikuwa anarejea nyumbani ambopo yalikuwa makazi yake wakati akiwa kocha mkuu wa Mbeya City aliyeipandisha daraja kucheza VPL na kuipa mafanikio ya kumaliza katika nafasi ya tatu katika msimu wao wa kwanza kwenye ligi kuu.
  • Yanga imepata matokeo ya ushindi katika mechi yake tano mfululizo kwenye ligi, (Yanga 1-0 Mtibwa Sugar, Yanga 2-1 Mgambo JKT, Toto Africans 1-2 Yanga, Stand United 1-3 Yanga na leo Mbeya City 0-1Yanga)
  • Yanga ndiyo timu pekee iliyofungwa mechi moja hadi sasa, ilifungwa na Coastal Union kwenye uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
  • Mbeya City wamepata ushindi mara mbili kwenye mechi zao tano zilizopita kwenye ligi (Mtibwa Sugar 1-0 Mbeya City, Mgambo JKT 0-1 Mbeya City, Mbeya City 4-0 Coastal Union, Majimaji 3-1 Mbeya City, Mbeya City 0-2 Yanga.
  • Donald Ngoma na Amis Tambwe ndiyo safu hatari zaidi ya ushambulizi msimu huu, wawili hao kwa pamoja wameshafunga jumla ya magoli 36 kwenye ligi. Tambwe akionoza orodha ya wafungaji bora kwa magoli 20 wakati Ngomba akiwa nafasi ya tatu kwa magoli yake 16.
  • Mbeya City imefungwa magoli mengi kuliko iliyofunga, imefungwa magoli 29 huku yenyewe ikifanikiwa kufunga magoli 26 na kufanya kuwa na -3 katika tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa.

No comments:

Powered by Blogger.