Prof. Lipumba: Uhaba wa Sukari Umesababishwa na Rais Magufuli

Akihojiwa na Mtangazaji Yvonne Kamuntu kwenye Azam News, Mchumi mbobezi hapa nchini
Prof. Ibrahim Haruna Lipumba amesema uhaba wa sukari uliopo kwa sasa nchini umesababishwa na Rais John Magufuli mwenyewe kwa kuzuia sukari ya nje kutoingizwa Nchini, ilhali viwanda vyetu havikidhi idadi inayohitajika katika uzalishaji wake.

Pia Prof. Lipumba amesema hakuna sheria inayoruhusu Serikali au Bodi ya Sukari kupanga bei ya sukari nchini hivyo ametaka siasa kuacha kutumika katika mambo serious na wafanyabiasahara wasitishwe.

No comments:

Powered by Blogger.