Sifa 10 za Mpenzi wa Kweli
Vijana wengi ambao wanapendana leo mapenzi yao hayadumu kiasi cha
kubatizwa jina la utamu wa
bazoka. Lakini yote hii inatokana na ukweli kwamba
elimu ya mapenzi ambayo ni muhimu kwa binadamu haitolewi ipasavyo.
Ipo zana potofu kwamba
kumfundisha mtoto mapenzi ni kumharibu, jambo ambalo si kweli bali inategemea
mtoto huyo anafundishwa nini na kwa wakati gani. Lakini cha kushangaza zaidi hata watu wazima ambao ni
wadau wa mapenzi hawayajui, matokeo yake wanajiingiza kwenye uhusiano wakiwa
bumbumbu na hivyo kuteshwa na changamoto zinazowakabili.
Leo tutajifunza kwa undani sifa kumi za mpenzi bora ili tuweze kuwatambua wapenzi wetu kabla ya kuwapa mioyo na utu wetu. Sifa hizo ni hizi zifuatazo.
Leo tutajifunza kwa undani sifa kumi za mpenzi bora ili tuweze kuwatambua wapenzi wetu kabla ya kuwapa mioyo na utu wetu. Sifa hizo ni hizi zifuatazo.
1: Mpenzi wa kweli ni yule ambaye hatangoja kujua nini unahitaji
yaani hana sababu ya kusubiri kuombwa ndiyo atoe msaada.
2: Ni yule atakayejua wakati gani huna furaha au una furaha na
atakuwa na wewe kwa hali zote mbili .
3: Ni yule atayekuwa tayari kukusikiliza kwa kile utakachosema,
hatojali umeongea baya au zuri .
4: Atakuwa na wewe wakati wa
shida na raha.
Hatakuwa mtu wa kuvizia vizia na kujisogeza wakati ukiwa na raha.
5: Mpenzi wa kweli atakuheshimu na hatopenda kuwa kikwazo cha
maisha yako, atakulinda daima.
6: Atakupenda kwa moyo wake wote na wala si kwa ajili ya
shinikizo fulani (pesa au mali)
7: Mpenzi wa kweli ni yule
atakayeonyesha kuthamini nafasi yako kama rafiki au mpenzi mbele ya wengine,
hafichi hisia zake mbele za watu, atakutetea na kukufanya wa kwanza.
8: Kwenye ukweli mpenzi mzuri atasema bila kukuficha na atapenda
kukuonyesha mifano ya namna ya kuwa mkweli na mwaminifu.
9: Mpenzi wa kweli ni yule anayejiamini, asiyeyumba
katika maamuzi hata kama atalazimika kufanya maamuzi magumu .
10: Atakuwa tayari kuvumilia,
hatakuwa mwepesi wa hasira wala kutumia lugha chafu na ubabe
No comments: