LEMA: WAZIRI ALINISHAURI NIFANYE FUJO ARUSHA ILI YEYE AINGILIE
GODBLESS Lema, Mbunge wa Arusha Mjini amesema kwamba, alishauriwa na George Simbachawene, Waziri wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kuwa, amfungie ofisini Athumani Kihamia, Mkurugenzi wa Jiji la Arusha ili kuibua vurugu na kisha (Simbachawene) aingilie, anaandika Charles William.Akizungumza bungeni leo asubuhi, Lema amesema Simbachawene alimtaka yeye na viongozi wengine wa Chadema wamfanyie vurugu mkurugenzi huyo kisha tukio hilo lioneshwe katika Runinga ili waziri aingilie kati mgogoro huo kwa madai, utakuwa umedhihirika.
“Nilimwambia Waziri Simbachawene kuwa Arusha tuna tatizo kwenye halmashauri tunaomba msaada, akanishauri tukafanye fujo ili aone kwenye vyombo vya habari na apate nafasi ya kuingilia mgogoro huo kwasababu rais amewapa nguvu wakuu wa mikoa.
“Akaniambia siwezi kuja kichwa kichwa nenda kafanye fujo, mfungieni mkurugenzi nje halafu mimi nione kwenye TV ili niingilie mgogoro huo. Yaani waziri anaogopa kuingilia migogoro katika halmashauri,” ameeleza Lema.
Katika hatua nyingine Lema ameendelea kumsakama Rais John Magufuli huku akiirejea tena kauli yake ya kumtabiria kifo kabla ya mwaka 2020 iwapo hatajirekebisha, kwa madai kuwa ameoneshwa suala hilo na Mungu kupitia maombi.“Mimi ni muombaji, nimeona maono kwamba rais asipojirekebisha Mungu kasema atakufa. Sasa hivi nina kesi nyingine ya hayo maono niliyoona lakini TB Joshua angeona wala isingekuwa kesi,” amesema Lema
No comments: