Maneno ya Rais Magufuli baada ya Dkt Shein kutangazwa kuwa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar


Kama ulipata taarifa za matokeo ya urais Zanzibar, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli
yalimfikia pia,  nakukaribisha kuzisoma sentensi Mbili za Rais Magufuli baada ya kupokea matokeo hayo…..
‘>>>Nakupongeza  kwa dhati Rais Mteule Dkt. Ali Mohamed Shein kwa ushindi ulioupata, ushindi ambao umeonesha kuwa wananchi wa Zanzibar bado wanahitaji uwaongoze kwa kipindi kingine cha miaka mitano‘
>>>’Ndugu zangu wa Zanzibar uchaguzi umekwisha, kilichobaki sasa ni kushirikiana na serikali yenu kuijenga Zanzibar na ninaamini mnao wakati mzuri wa kuijenga Zanzibar yenye maendeleo chini ya uongozi wa Dkt. Ali Mohamed Shein‘


No comments:

Powered by Blogger.