Rais Magufuli atekeleza agizo la Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam baada ya kuhakikiwa silaha zake
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amekuwa mtu wa kwanza kutekeleza agizo
la Paul Makonda ambaye ni mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam la kuhakikisha silaha, ambapo bunduki zake mbili aina ya Shortgun na Pistolzimehakikiwa nyumbani kwake Ikulu Dar es Salaam.
Hizi ni baadhi ya picha za Rais Magufuli akiwa katika zoezi la kuhakikiwa silaha zake.
\ Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt.
John Pombe Magufuli akiweka dole gumba katika moja ya fomu za
uhakiki Ikulu jijini Dar es Salaam. Picha na IKULU
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John
Pombe Magufuli akiitoa silaha
yake aina Bastola kwa ajili ya uhakiki Ikulu jijini Dar es Salaam.
Kamanda wa Kanda
Maalum ya Mkoa wa Dar es Salaam Kamishna CP
Simon Sirrokulia akimkabidhi silaha aina ya shortgun Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt.
John Pombe Magufuli mara baada ya uhakiki uliofanyikaIkulu jijini
Dar es Salaam.
Picha:Michuzi
No comments: