BREAKING:Jana usiku kuna Ndege imekamatwa ikisafirisha nyani, Maamuzi yametangazwa leo


Habari niliyoipokea muda mfupi uliopita zinamhusu Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof Jumanne Magembe kumsimamisha kazi Mkurugenzi
msimamizi wa wanyama pori  Charles Mulokozi kwa kutoa vibali vya kusafirisha wanyama kwenda nje pamoja na wakurugenzi wanne wa Huduma za misitu kutokana na usafirishaji na uvunaji  holela wa magogo.
Akizungumza na kituo cha ITV Waziri Magembe amesema….>>>watu wanavuna mazao ya misitu kule kalambo, tukaenda kule tukakutana na  magogo mengi sana yako msituni ambayo yanatakiwa yawe yamelipiwa na hayakulipiwa, nimewaondoa hili tuweke uongozi mpya kwa sababu kinachoonekana ni kwamba hawana uwezo wa kuongoza’
Kuhusu kumsimamisha kazi Mkurugenzi msimamizi wa wanyama pori  Charles Mulokozi, Waziri Magembe amesema .…..>>>Jana usiku tumekamata ndege ambayo ilikuwa inasafirisha nyani, inaonekana ni biashara inayofanywa kwa hiyo amesimamishwa kazi, uchunguzi ufanywe ili tuone hili jambo la kusafirisha wanyama nje ya nchi limefanywa kiasi gani na ni nani anafanya’
I

No comments:

Powered by Blogger.