Producer Scott Storch wa Marekani hakupenda kuona Mtanzania Lamar kapost beat yake Instagram? tazama comments zake
Usiku wa February 23 2016 Producer
Mtanzania Lamar alipost video akiwa studio kwake na
spika zikitoa mdundo mmoja mkali alafu akaandika caption yenye swali, watu
wacomment kumwambia Msanii gani atafaa kupita juu ya huo mdundo kisha akamtag
producer Scott Storch kwamba ndio anampa Inspiration, yani
kazi ya Scott inamvutia na anajifunza vingi kutoka kwake.
Kabla
ya yote inabidi ufahamu kwamba Scott Storch (42 yrs) ni producer maarufu wa
Marekani ambaye mikono yake ilihusika kuzitengeneza beats za hits nyingi
ikiwemoNaughty Girl
ya Beyonce, Sorry ya Rick Ross na Chris Brown, pia Make
It Rain ya Fat Joe na Lil Wayne.
Kanye
West na Scott
Sasa comment ya kwanza ya Scott baada ya kuona hii post ya Lamar ni swali, Kwanini
unaweka beat zangu kwenye Instagram yako? Lamar akamjibu… karibu
kwenye ulimwengu wako boss, mimi ni shabiki wako mkubwa, endelea
kutu-inspire, Scott akamjibu.. tafadhali
naomba usipost beat zangu ukajidai ni wewe umezitengeneza.
Baada ya hapo Lamar alimjibu... ‘Hakuna matata boss, haitatokea
tena‘ na Watanzania
wengine wakaanza kucomment akiwemo producer Mtanzania Lucci, wasanii Dogo Janjana Julio
Batalia
No comments: