Baraka da Prince akasirishwa kuona Linex kasema amefanya upuuzi kusambaza video ya Mwanamke Whatsapp
Kupitia kwa Soudy Brown kwenye
YOU
HEARD ya CloudsFM,
mwimbaji staa wa bongofleva Linex alihojiwa kuhusu ishu inayoendelea
kwenye mtandao wa Whatsapp ya kusambazwa kwa video ya mpenzi mpya
wa Linex akionekana mapenzini
kitandani na mwimbaji Baraka Da Prince ambaye anatajwa kuwa mpenzi wake wa
zamani hivyo Baraka anatuhumiwa kuisambaza hiyo video.
Baada ya hii ishu kumfikia Baraka,
ameongea kwenye Exclusive na AyoTV na kusema ‘Sijawahi kutembea na mtu ambaye
katembea na Linex…. kwanza hawezi kutembea na mtu ambaye mimi natembea nae,
yeye labda ndio anataka hiyo kiki ila mimi siwezi kutaka kiki kwa Linex, Linex
kanikosea‘
No comments: