Njia 4 za Kumvutia Mwanamke Hata Kama Huna Pesa
Kutokana na hali
halisi ya maisha yetu
, sote tunatambua ya kuwa mwanaume
huvutia zaidi anapokuwa na pesa;
gari la kifahari litakuongezea mvuto, nguo nzuri zitawafanya wanaweke
wakugeuzie macho yao kila kona, na
kama una pesa ndio utawanasa kwa urahisi sana.
Kama unakumbuka Chris Brown alitoa wimbo wake
unaojulikana kwa jina la “loyal“ na
uliwashika watu wengi sana hususani vijana, kwa kuwa ulibeba
ujumbe wa jinsi gani mwanamke asivyoonyesha upendo kwa mwanaume asiye na pesa, lakini vilele alieleza jinsi
gani mwanamke anavyoonekana kuonyesha upendo kwa mwanaume mwenye pesa.
Hata hivyo, Naamini kwa dhati kuwa pesa ina
nafasi kubwa katika kumfanya mwanaume avutie zaidi, wanawake
wanaweza pia kuvutiwa na wewe kama una baadhi ya sifa hizi
hapa chini.
Wanawake
kwa namna fulani huweza kumtambua mwanaume kama ni mkweli au lah! na kama
mwanaume utaonekana kuwa mkweli, kwa asilimia kubwa utawavutia
wanawake wengi. Usimzunguke mwanamke na kumweleza mambo ya
uongo juu yako, au kumwonyesha darili zozote za uongo ndani yako. Kama utakuwa
mkweli mbele yake una asilimia mia moja ya kumvuta kwako.
Jambo jingine la muhimu ni
kujiamini; moja ya makosa makubwa ambayo hufanywa na wanaume wasiomiliki
akaunti kubwa benki ni hali ya kutojiamini, imani humfanya mtu asimame imara na
pia atoe mwangaza katika utendaji wake; kumbuka usipojiamini mwenyewe hakuna
atakayewezakukuamini.
3. Jifanyie sehemu ya mauzo.
Mimi
naamini sana katika jambo hili; kama unaweza kumfanya mwanamke
acheke, hiyo ni sehemu yako ya mauzo binafsi itakayomvutia mwanamke kwako. Kama
una kipaji au ujuzi wowote kama vile kuimba, hiyo ndiyo sehemu yako ya mauzo.
Ingawa usitumie sehemu yako ya mauzo kupita kiasi, nikimaanisha kuwa utumie
kipaji chako kuonyesha ubora wako na si vinginevyo.
Wanawake
pia huvutiwa na udadhifu wa mtu; kama hauna pesa jitahidi
basi hata kuwa nadhifu kwaajiri yako mwenyewe. Kama
uko nadhifu kimwili na kiakili, katika hali ya mazingira fulani mwanamke
atavutiwa nawe. Unadhifu ni jambo linalopendwa na kukubalika na wanawake
wengi hivyo kama utajitahidi kuwa nadhifu, hata kama hauna pesa nyingi
wanawake watavutiwa na wewe bila shaka.
Je,
unadhani unaweza kumvutia mwanamke hata kama hauna kitu?
No comments: