Kauli Mbili za Zitto Kuhusu Mali na Madeni ya Viongozi..Amtaka Rais Aamuru Ziwekwe Kwenye Mtandao Kila Mtu Aone

Zitto Amefunguka Haya kwenye ukurasa wake wa
Facebook
"Rais
Magufuli aagize Mali na Madeni ya Viongozi yawekwe wazi kweny tovuti ya Tume ya
Maadili ya Viongozi ( sheria irekebishwe kuzuia watu wanaoona matamko kuziweka
wazi, bila uwazi ni vigumu kupambana na rushwa)"
"Taarifa
kwamba kuna Mawaziri ambao hawakujaza fomu za Maadili au kuficha mali zao katika
tangazo la Mali na Madeni ni jaribio kubwa kwa Rais Magufuli kuhusu dhamira
yake ya kupambana dhidi ya Ufisadi. Sheria ya Maadili ya sasa, licha ya udhaifu
wake, ikitekelezwa ( enforced) ni silaha bora ya kuweka misingi ya Maadili
katika Uongozi wa Umma"Zitto Kabwe
No comments: