Diva Loveness Ahusishwa Katika Utapeli wa Kudhulumu Mtoto Kilema Aliyechangiwa na Wadau Kupitia Kipindi Chake

Diva Amejikuta Katika wakati mgumu
baada ya Dada mmoja anajiita Ms_Resty
huko instagram kumrushia shutuma za kung'ang'ania shilingi laki saba za msaada
zilizochangwa na watu kumsaidia mtoto kilema kupitia kipindi cha Ala za roho
cha anachokiendesha radioni...Mpaka sasa Diva hajasema chochote kuhusu tuhuma hizi alizoangushiwa...
Dada huyu amepost hivi...

From
@Ms_Resty - Jamani jamani Loveness Loveness aka Diva the bawse mbona hauendani na
jina lako linalomaanisha Upendo??? Huu sio Upendo kumsaidia mtu haimniishi ndo
uchukue pesa zake!!! Kumsaidia mtu haimanishii ndo umuonee kwa vile wewe ndo
ulimtangaza kwenye kipindi chako! Anyway sijawai kuwa na mazoea na huyu dada
ila kuna siku nilisikilizaga kipindi chake nikamsikia anamtangaza yule mama
ambaye alikuwa na mtoto hana haja kubwa wala mguu mmoja nikaguswa kwa vile mimi
pia nilishaakaga maeneo ya kawe nikaend kumuona nikampost apa Insta kumuombea
msaada watu wakanisaidia kupost na wengine kutuma michango mbalimbali! Pesa ni
pesa jamani mi sikutaga kukaa nazo ndo maana nikaweka namba yake hata wale
baadhi walionitumia nilizituma pale pale kuepusha kuzitumia! Jamani sasa Diva
wa Clouds @divathebawse kipindi cha Ala Za Roho ambaye ndo alimtangaza akwambia
ampe pesa zote alizochangiwa ili yeye ndo awe anampatia kdg kdg huyo Mama Husna
mama husna akumpa zote sababu nyingine tulizitenga ili tuulipie ule mguu wa
mtoto akampa laki 7 akamwambia kwa vile yeye anafoundation na hayupo mwenyewe
ndani ya iyo foundation atakuwa anampa kdg kdg anunue vifaa vya mtoto! Vifaa
vimeisha Diva hataki kutoa pesa anasema huyo mama kamuongelesha vibaya na yeye
ndo aliyemtangaza so itatumika kwenye charity nyingine! Sikumuelewa kabisa
nikamwambia basi mimi namuombea msamaha huyu mama kama alimkosea ila pesa
ampatie Diva kagoma! Hii sio sawa ni uonevu kumbuka baada ya mimi kupost ndo
ilicreate Big awareness kwa watu wengine wakachanga sasa atachukuaje pesa za
michango ya mtoto mlemavu mwenye matatizo agome kurudisha naombeni msaada
jamani ubinadamu kazi! Na siku zote tenda wema uende zako! Hata angepata ngapi
mwache apatemaana kumlea yule mtoto jamani sio lelemama!! Naombeni Diva atoe
pesa nimemuomba ikashindikana na ndo maana nikaamua kuipost uku-Ms_Resty
My Take:
Ni vizuri Diva ajitokeze na kujibu tuhuma hizi ambazo zinazidi kusambaa mitandaoni...
My Take:
Ni vizuri Diva ajitokeze na kujibu tuhuma hizi ambazo zinazidi kusambaa mitandaoni...
No comments: