Jerry Muro Atoa Mpya ''Simba si Washindani Wetu Tena...Watabaki Kuwa Watani Wetu Kama Wagogo na Wasukuma

Klabu ya soka ya Yanga imetangaza rasmi
kuwa kuanzia leo wekundu
wa Msimbazi Simba si washindani wao tena bali ni watani wa jadi kama walivyo
wasukuma na wagogo.
Tamko hilo limetolewa hii leo na mkuu wa idara ya habari na
mawasiliano wa wanajangwani hao Jerry Muro wakati akitoa salam za pongezi kwa
wachezaji, benchi zima la ufundi na wanachama kwa kufanikisha kile
walichokifanya Jumamosi iliyopita kwenye mtanange wa ligi kuu ya soka Tanzania
Bara walipoinyuka 2-0 Simba.
Aidha Muro ameongeza kuwa kwa sasa wanachotazama ni shughuli tatu
zilizo mbele yao mechi ya kombe la shirikisho dhidi ya JKT Mlale, mchezo wa
klabu bingwa barani Afrika dhidi ya Cercke de Joachim ya Mauritius na mechi
dhidi ya Azam ikiwa ni ya ligi kuu Tanzania bara.
Aidha amesema kuwa kikosi cha Yanga kimeanza mazoezi katika uwanja
wa chuo cha polisi Kurasini kwa ajili ya mchezo wa kombe la shirikisho dhidi ya
JKT Mlale Jumatano na mara baada ya mchezo huo kitaendelea na maandalizi ya
mechi ya marudiano dhidi ya Cercle de Joachim.
No comments: