Breaking News: TCU Yakifuta Chuo Kikuu cha St. Joseph Kampasi ya Arusha.......Wanafunzi Watahamishiwa Vyuo Vingine

1.Tunapenda kuuarifu
umma kwamba, Chuo Kikuu cha Mt. Yosefu
Tanzania (SJUIT) Kampasi ya Arusha ni
mojawapo ya vyuo vikuu vilivyosajiliwa na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU)
ambacho kilianza kudahili wanafunzi kwa mara ya kwanza mwaka wa masomo
2013/2014.
2.Kwa mujibu wa
kifungu cha 5(1) cha Sheria ya Vyuo Vikuu, Sura ya 346 ya Sheria za Tanzania,
Tume ina mamlaka ya kusimamia na kudhibiti ubora na usimamizi wa uendeshaji wa
Vyuo Vikuu hapa nchini.
3.Kwa muda mrefu na
kwa wakati tofauti kumekuwapo na matukio ya migogoro baina ya uongozi wa Chuo
Kikuu cha Mt. Yosefu Kampasi ya Arusha na wanafunzi.
Kwa kipindi hiki chote
Tume imekuwa ikifuatilia kwa karibu chimbuko la migogoro hiyo na kuchukua hatua
stahiki ikiwa ni pamoja na kutoa maelekezo kwa uongozi wa chuo kurekebisha
kasoro zinazosababisha migogoro chuoni hapo.
Kwa sehemu kubwa
migogoro hiyo imekuwa ikitokana na matatizo ya ubora, uongozi, ukiukwaji wa
sheria na taratibu za uendeshaji wa chuo kikuu kama zilivyobainishwa na Sheria
ya Vyuo Vikuu.
Hata hivyo jitihada za
Tume ya Vyuo Vikuu kukitaka Chuo Kikuu cha Mt. Yosefu Tanzania (SJUIT) Kampasi
ya Arusha kuhakikisha kuwa elimu inayotolewa katika Kampasi hii inakidhi
viwango vya ubora vilivyowekwa na Tume hazikupewa uzito stahiki na uongozi wa
chuo.
4.Hivi sasa Kampasi ya
Arusha ina jumla ya wanafunzi 1557 wanaosoma programu za masomo ya ualimu wa
sayansi zifuatazo:

1.Tunapenda kuuarifu
umma kwamba, Chuo Kikuu cha Mt. Yosefu Tanzania (SJUIT) Kampasi ya Arusha ni

PROF. YUNUS D. MGAYA
Katibu Mtendaji
Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania
26 Februari 2016
No comments: