Breaking News: Rais JPM kuwatema mawaziri 4 na naibu waziri 1,tazama apa

Rais John Pombe Magufuli ametoa muda mpaka
leo jioni kwa Mawazri wanne
na Naibu waziri mmoja ambao hawajarejesha fomu kwa
Sekretarieti ya maadili kwa ajili ya kuanisha mali na madeni wanayodaiwa
ambapo wamepewa muda
mpaka saa 12 jioni wawe wamesharejesha fomu hizo
Mawaziri wanaotakiwa
kurejesha fomu za tamko la rasilimali pamoja na hati ya ahadi ya uadilifu ni
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Bw. Charles Kitwanga na Waziri wa Nchi (OMR –
Muungano na Mazingira), Bw. January Makamba. Wengine ni Waziri wa Mambo ya Nje,
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Ushirikiano wa Kikanda na Kimataifa, Dk.
Augustine Mahiga ambaye anatakiwa kurejesha hati ya ahadi ya uadilifu kwa
viongozi wa umma na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Prof. Joyce
Ndalichako ambaye anatakiwa kutoa tamko la rasilmali na madeni.
“Mheshimiwa Rais
ameelekeza mawaziri ambao hawajajaza tamko la rasilmali au hati ya ahadi ya
uadilifu wafanye hivyo na kuzirejesha kabla saa 12 jioni na Waziri ambaye
atashindwa kutekeleza agizo hili atakuwa amejiondoa mwenyewe kwenye nafasi
yake,” amesisitiza Waziri Mkuu.
Waziri Mkuu amesema
wakati akifungua mafunzo ya Mawaziri na Naibu Waziri kuhusu Mwongozo wa Maadili
ya Viongozi wa Umma na Utekelezaji wa Ahadi ya Uadilifu yaliyofanyika Ikulu
jana (Alhamisi, Februari 25, 2016) alikabidhiwa majina ya Mawaziri na Naibu Mawaziri
ambao hawajawasilisha Tamko la Rasilimali na Madeni kwa Kamishna wa Maadili.
source:Eatv
No comments: