Uzinduzi wa cheza kwa madoido wafana Dar Live!
Yamoto Band wakizindua rasmi video yao mpya inayofahamika kwa jina la Cheza kwa Madoido katika Ukumbi wa Dar Live uliopo Mbagala, Zakhem jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo.
Msanii wa Bongo Fleva, Hellen George ‘Ruby’ akifanya yake stejini.
…Ruby akiimba wimbo wake ‘Na Yule’.
Msanii wa Bongo Fleva, Shetta akitoa burudani kwa mashabiki wake.
Shetta akiendelea kuwapa burudani mashabiki zake.
Chegge na Temba wakikamua stejini.
…Chege akiendeleza makamuzi.
Queen Darleen akitoa burudani kwa mashabiki wake.
Mwimbaji wa Moyo Modern Taarab akiimba jukwaani.
Bendi ya Moyo Modern Taarab ikitoa burudani.
Mpiga kinanda wa Moyo Modern Taarab akifanya yake.
Madansa wakifanya yao ndani ya ukumbi wa Dar Live jana usiku.
VIJANA wanaounda Bendi ya Yamoto, usiku wa kuamkia leo wameangusha burudani ya aina yake katika Ukumbi wa Dar Live, Mbagala-Zakhem jijini Dar wakati vijana hao wakizindua rasmi video yao mpya inayofahamika kwa jina la Cheza kwa Madoido.
Kabla ya uzinduzi wa Cheza kwa Madoido, wasanii mbalimbali walipanda jukwaani kutoa burudani ikiwemo bendi mpya ya Taarab iitwayo Moyo Modern Taarab inayomilikiwa na kiongozi wa Yamoto Band, Said Fela.
Wasanii mbalimbali wa chipukizi nao walipata nafasi ya kuonesha vipaji vyao kwa kuimba nyimbo mbalimbali ambapo wapenzi wa burudani waliburudika vya kutosha.
Katika listi ya wasani waliotumbuiza jukwaani ni pamoja na Ruby, Dulla Yeyo, Izeman huku Moyo Modern Taarab wakipagawisha na nyimbo zao kali zinazojulikana kama Haijalishi, Dongo la Gizani na Zetu Duwa.
Wengine waliokamua jukwaani ni Chegge, Temba, Queen Darleen, Shetta, Ditto na wengine kibao kisha uzinduzi wa Cheza kwa Madoido kufanyika katika ‘skrini’ kubwa kisha Yamoto Band kutumbuiza shoo kali
No comments: