Mlela akiri kuponzwa na starehe!
YUSUF Mlela ‘Angelo’ amekiri kurudishwa nyuma kimaendeleo kutokana na kuendekeza sana starehe siku za nyuma, ikiwemo ulevi kupindukia na kubadili wanawake.
Akizungumza kwa njia ya simu Jumanne ya wiki hii katika mazungumzo ya kawaida na mwandishi wetu, Mlela alisema kila wakati alikuwa akigombana na mama yake mzazi juu ya suala hilo na kuona kama anaonewa lakini kwa sasa amekua na kuona madhara ya starehe hususan baada ya kuanza kuandamwa na majukumu ikiwemo kusomesha.
“Dah, kwa sasa nimeacha kabisa mambo ya pombe na wanawake, unajua vimeniponza sana, kila mara nilikuwa nikigombana na bi mkubwa (mama mzazi), na kuona kama ananibana vile, sasa majukumu yananiandama, nasomesha ujue, kwa hiyo nalazimika kubadili mfumo mzima wa maisha yangu,” alisema Mlela.
No comments: