DIAMOND PLATNUMZ AKUMBWA NA MPASUKO NDANI YA FAMILIA YAKE
Mwandishi wetu
Breaking news! Saa chache kabla ya ile sherehe ya kukata na shoka ya 40 ya mtoto wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Latifah Nasibu ‘Princess Tiffah’ inayotarajiwa kufanyika mapema kesho, ndani ya familia hiyo kunadaiwa kuibuka bonge la mpasuko.
Habari kutoka kwa chanzo makini ndani ya familia hiyo yenye maskani yake nje kidogo ya Jiji la Dar, maeneo ya Madale-Tegeta zilieleza kuwa, kuna madai mazito ya usengenyaji ambayo yametawala yanayodaiwa kutia doa katika shughuli hiyo ya kesho.
NI MAMA DIAMOND NA ZARI
Habari hizo za kidaku zinadai kwamba, mama mzazi wa Diamond, Sanura Kassim ‘Sandra’ yuko kwenye sintofahamu na mwandani wa mwanaye, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ kwa kile kilichoelezwa kuwa ni mambo ya umbeya.
KAMERA ZABUMBURUA
Chanzo hicho kimelieleza gazeti hili kuwa, hivi karibuni, Zari, kupitia kamera za ndani ya nyumba hiyo, Close Circuit Television (CCTV), alibaini picha zikimuonesha Mama Diamond na mwanaye wa kike ambaye ni dada wa Diamond aitwaye Esma Platnumz wakiwa kwenye mazungumzo na muonekano wa kumseng’enya, jambo ambalo lilimkera kupitiliza.
ZARI ATAKA KUONDOKA NA TIFFAH
Mpashaji huyo aliendelea ‘kuponyokwa’ na maneno kuwa, baada ya kubaini jambo hilo, Zari amekuwa katika harakati za kutaka kuondoka nchini kwenda kwao kwa kile alichokiita ‘kujiepusha na ya walimwengu’ kabla hata mwanaye, Tiffah hajafanyiwa pati yake ya kutimiza siku 40 tangu kuzaliwa kwake.
“Hapa nyumbani hali si shwari kabisa, Zari hajapendezwa na kitendo hicho, siku zote amekuwa akiishi nao kwa upendo akiamini ni watu wema kwake, sasa anashanga tena kuwepo kwa hali ya majungu na manenomaneno.
“Nasikia amefikia hata hatua ya kulazimisha kuondoka Bongo na mwanaye,” kilisema ‘kikulacho’ hicho.
MPASUKO?
Chanzo hicho kiliendelea kutiririka kuwa, kitendo hicho kimesababisha mpasuko mkubwa kwenye familia ya Diamond kwani kuna baadhi ya wanafamilia wapo upande wa Zari na wengine wapo upande wa Mama Diamond na Esma.
HUYU HAPA MAMA DIAMOND
Baada ya kujazwa ubuyu huo wa motomoto, muda mfupi kabla ya kwenda mitamboni, gazeti hili lilimtafuta Mama Diamond na kumuuliza juu ya ishu hiyo ambapo alikanusha vikali kwa madai kwamba hayo ni maneno ya umbeya kisha akakata simu.
MAMA DIAMOND ADONDOSHA KIMOMBO
Hata hivyo, alipoendelea kupigiwa ili afafanue maswali ya mwandishi, Mama Diamond alituma ujumbe mfupi wa maneno kwa kimombo.
Mama Diamond: Iam driving (naendesha gari).
MAANDALIZI YA SHUGHULI USIPIME
Hata hivyo, wakati hayo yakiendelea, maandalizi ya shughuli ya Tiffah yalikuwa yamekamilika kwa kila kitu huku ndugu wa Zari wakiwa wameshafika nyumbani hapo wakiongozwa na Mama Zari, Halima Hassan.
Hatimaye, Diamond na Zari walifikia makubaliano ya kufanyia shughuli hiyo nyumbani hapo baada ya kuwepo kwa msuguano mkali kufuatia makampuni ya bidhaa za watoto kutaka ifanyikie kwenye ukumbi
No comments: