Mange Kimambi Aongelea Issue ya Wimbo Mpya wa Roma Kutaka Kufungiwa 'Lini Tanzania Hii Mshawahi Sikia nyimbo ya Propaganda za Kisiasa Inapigwa redioni au TV?'


Issue ya Roma.. Kabla sijaanza wangapi wameiski radioni nyimbo ya
Diamond kumsifia Magufuli??? Nyoosheni mikono? Au nyimbo ya Kiba akimsifia Magufuli? Wakangapi mmesikia?? Okay kumbe Jibu mnalo.... Kama kawaida yetu wabongo kudandia Treni kwa mbele. 
Hivi Kweli mlidhani hii nyimbo kuna radio itapiga.? Hata Mengi mwenyewe na uchadema wake hawezi kupiga. Yani Huyu msanii hakuona Muda wa kutoa huu wimbo Hadi kipindi cha Uchaguzi?? ____________________________
Yani maredio wapige nyimbo za kampeni? Yani nyie watu mnachekesha mpaka mnatia huruma. Mnavyojifanya victims of the system sasa , Yani mtu anaweza dhani Tz kuna nini sijui.... Ila mnachokitafuta mtakipata soon. Hivi Kweli nyimbo Kama hii inaweza kupigwa sehemu?? Au sio mnatafuta tu vitu vya kulalamika? Yani mnajitia Kama watu wa South Korea. Maana mnavyojifanya mko oppressed kha!!! Embu msituchafulie uchaguzi na ujinga wenu. Mmeshaanza kutafuta visababu vya kundamana.... Huyu msanii nae alikuwa anatafuta pakutokea tu., Kwenda kutoa nyimbo ya Propaganda za siasa Tena kipindi cha uchaguzi mnadhani alikuwa hajui haitochezwa? Alijua sana. Mie nilikuwa hata sijui Ana exist Ila hii nyimbo Kila mtu atamjua. He is smart aisee. ------------ ___________________________________
Yani mmekuwa wanafki mpaka mnauziii, lini Tanzania hii mshawahi Sikia nyimbo ya Propaganda za kisiasa inapigwa redioni au TV? Mnajua haiwezekani Ila mnatafuta sababu za kuwahamasisha watu kuwa CCM wanawaonea..... Hamumpati mtu...

Source: Mange Kimambi

No comments:

Powered by Blogger.