Lowasa Maalimu seifu wavunja rekodi zanzibar

Kampeni za kuwania urais wa Zanzibar kupitia chama cha wananchi CUF zimeanza rasmi leo Zanzibar huku mgombea wa urais kupitia chama hicho Maalim Seif Sharrif Hamad akitangaza na kuahidi mabadilko makubwa ya utendaji na kiuchumi endapo wazanzibari watampaa ridhaa ya urais.


Akiwahutubia maelfu ya wanachama,wapenzi na wananchi waliofurika katika uwanja wa demkrasia akiwemo mgombea urais wa jamhuri ya muungnao kupitia umoja wa UKAWA Mhe Edward Lowassa,viongozi wa vyama vya umoja huo NLD,NCCR Mageuzi na Chadema na viongozi waandamizi wa chama hicho Maalim Seif ambaye pia ni makamu wa kwanza wa rais amesema serikali atahakikisha anawaletea mabadiliko makubwa ya wananchi kiafya, kielimu na kijamii huku akiahidi kuweka utawala wa sheria.

Akizungumzia suala la uchumi Maalim Seif amesema serikali yake italivalia njuga suala la mafuta kwa uadilifu na kuweka maslahi ya wazanziabri mbele huku akiahidi serikali yake itabadilisha mfumo na kuwa na mfumo unaotakiwa na wananchi ikiwemo suala la muungano na katiba.

Mapema mgombea urais wa muungano Edward Lowassa katika salamu zake amewataka wananchi wa Zanzibar kuleta maabdilko na kuendeleza kampeni za ustarabu na yeye akiahidi kutoa ushirikiano wa dhati kwa Maalim Seif kwa vile ni kiongozi anayefaa kuwa rais wa Zanzibar, huku msaidizi wa kampeni wa chama hicho Mansour Yussuf Himid amesema umefika wakati wa Zanzibar kuleta mabadiliko na wasikubali kwa vile uongozi ulioko madarakani sasa hauna nia ya kulinda na kuendeleza mapinduiz ya Zanzibar.

Kuanza kwa kamepni hizo ni ishara za kuanza harakati za uchaguzi kwa vyama mbalimbali wakati cuf wanaelekea Pemba, vyama vyingine vilivyoweka wagombea nao vinaanza kampeni zao kuanzia kesho huku chama tawala cha CCM wao wataianza rasmi jumapili katika uwanja huo wa demkrasia, huku hadi tunaleta taarifa hizi kampeni hizo za leo zimekwisha kwa salama na amani.

Angalia Video wakati wa Uzinduzi hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.