Mahaba niue: Riyama laivu
KANASWA! Staa wa filamu Bongo, Riyama Ally kwa mara ya kwanza amenaswa laivu na kijana aliyemtambulisha kama mwandani wake, akimtaja kwa jina la Idd Mwalimu Mzee, anayemzidi umri kwa miaka saba, Amani linaandika.
‘Sapraizi’ hiyo ilitokea saa sita mchana Jumatatu wiki hii nyumbani kwa muigizaji huyo, Mabibo jijini Dar, akiweka wazi kuwa muda wowote kuanzia sasa watafunga ndoa, kwani anampenda kwa dhati mpenziwe huyo, aliyesema ni msanii wa muziki wa Kizazi Kipya, akifanya Hip Hop.
“Yeah, huyu ndiye mchumba wangu kipenzi, anaitwa Idd Mwalimu Mzee ingawa anajulikana kwa wengi kama Leo, ni msanii wa muziki, nampenda sana jamani japo ninamzidi umri kwa zaidi ya miaka saba, lakini umri siyo tatizo kabisa,” alisema Riyama aliyekuwa akicheza na mtoto wake sebuleni, akiwa amekaa kimahaba na mahabuba wake huyo.
Riyama ambaye amejizolea umaarufu mkubwa kutokana na uwezo wake wa kuigiza kwa umahiri karibu kila sehemu anayopangiwa, pia amejijengea heshima ya kutoandamwa na skendo za mapenzi kama walivyo mastaa wengine wa hadhi yake
No comments: