sababu za Alikiba kutotokea jangwani

U hali gani Ali Kiba? Natumai u mzima kabisa na unaendelea vyema na shughuli zako za muziki.
Mimi kama shabiki/mpenzi na mfuasi wako napenda kukupongeza kwa kitendo chako cha kishujaa na chenye hekima cha kutokuhudhuria kwenye mkutano wa kuzindua kampeni na ilani za chama cha CCM uliofanyika leo jijini Dar Es Salaam

katika viwanja vya Jangwani.

Leo mchana nilisikia tetesi kuwa utakuwepo jangwani, niliumia sana.
Niliamua kusitisha shughuli zangu zote leo ili niweze kuangalia mkutano huo niweze kuona kwa macho yangu kama utaweza kufanya onesho kwenye mkutano ule au lah!

Lakini hadi mwisho wa mkutano sijakuona kabisa, kwa hili nakupongeza sana Ali Kiba. Umenipa sababu za kukupenda na kuzidi kuupenda muziki wako mara dufu.
Kila mara huwa nasema kuwa siupendi mziki wako tu, bali na mtindo wako wa maisha kiujumla.

Tunapoongelea suala la msanii ni kioo cha jamii, wewe ndiye hasa unayefaa kuitwa kioo cha jamii.
Busara na hekima zako Mungu alizokujalia na kipaji chako ni tunu ya kipekee....hongera sana.

Naomba hekima hizo zisiishie kwenye mkutano wa leo tu, bali mikutano yote inayohusu chama cha CCM. Sitaki kuzungumzia hili zaidi maana hakuna Mtanzania mwenye akili timamu anayeweza kuwaunga mkono viongozi na chama hiki kiujumla.

Naomba usinitie aibu mimi na mashabiki wenzangu kama yule mwenzio alivyowatia aibu na kuwakera mashabiki wake kwa kitendo chake cha kuonesha mahaba yake hadharani juu ya chama dhalimu cha Mapinduzi na mgombea wake Magufuli.

Kwa hili, nasema ASANTE SANA.
NAKUSHUKURU NA KUKUAHIDI KUWA SHABIKI WAKO MILELE!
MUNGU AKUBARIKI.

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

No comments:

Powered by Blogger.