kisa lowasa Jacqueline wolper

MTOTO mzuri Bongo Movies, Jacqueline Wolper, amejikuta akiambulia matusi mazito kutoka kwa staa mwenzake Isabela Mpanda kisa kikiwa ni kuonesha mapenzi yake kwa mgombea urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa.Kisa Lowassa, Wolper Aoga MatusiIsabela aliamua kumtusi staa huyo akidai anamshanga kujinadi kila siku katika mtandao wa Instagram kuwa ni mfuasi wa Lowassa wakati amelelewa na Chama cha Mapinduzi (CCM)
.Kupitia mtandao huo wa Istagram, Isabela aliamua kumtolea uvivu Wolper hadharani kwa kumwambia aache kupotosha umma kwamba ana mapenzi yaliyopitiliza wakati ni mnafiki mkubwa kwani upande wa pili anaitegemea CCM iliyomlea kisiasa Lowassa kabla ya kuhamia Chadema.“Huyu naye paka gani (Wolper) anajitia anaiponda CCM wakati njaa zake anaponea CCM. Panya Road wewe kwani anafanya nini koko huyu mpuuzi mkubwa, ms…,” aliandika Isabela kwenye Instagram.Baada ya Isabela kumporomoshea matusi hayo, mtu wa karibu na Wolper alidai suala hilo lilimnyima raha kiasi cha kujuta kuonesha mapenzi yake kwa Lowassa.“Wolper amejuta. Amesikitishwa na matusi hayo ambayo ameyaona hayakumstahili,” alisema mtu huyo wa karibu na Wolper.Alipotafutwa Wolper kuhusiana na ishu hiyo, alikiri kuona matusi hayo na kudai alimpuuza maana si mtu wa hadhi yake.“Mpuuzi huyo. Nimempuuza maana hata simu yake anayotumia kuandikia huo ujinga na yangu hazifanani. Simu yangu haina hadhi ya kumjibu mtu mwenye simu za kimaskini,” alisema Wolper.Chanzo: GPL

No comments:

Powered by Blogger.