wema amtangazia maimatha bifu mwanzo mwisho wafikishana polisi
Staa wa filamu, Wema Sepetu
Mwandishi Wetu
KUMEKUCHA! Hivyo ndivyo unavyoweza kusema kufuatia mtifuano kati ya mtangazaji maarufu wa televisheni, Maimartha Jesse na staa wa filamu, Wema Sepetu baada ya bifu la wawili hao kufika jeshi la polisi.
Akipiga stori na gazeti hili, Maimartha alisema Wema alikuwa na nia ya kumdhalilisha kwani baada ya kumtafuta na polisi na kumkosa, waliamua kumpigia simu na kumuita kituoni Kijitonyama (Mabatini) ambako alisomewa mashtaka ya kumtukana Wema katika mtandao wa kijamii wa Instagram.
Mtangazaji maarufu wa televisheni, Maimartha Jesse
“Yaani Wema alitaka kunidhalilisha ndiyo maana polisi walikuja kibao kwenye gari lao hapa dukani kwangu na waliponikosa ndiyo wakanipigia simu kwamba niende mwenyewe kituoni, nikaenda nikatoa maelezo yangu ila sasa nitakula naye sahani moja kwani watu wake wanaendelea kunitukana sana mtandaoni nami siwezi kukubali,” alisema Maimartha

No comments: