Wakala_wa_Shetani - 5
KWA TAARIFA
ZAIDI NICHEKI HAPA 0785848566
ILIPOISHIA
Kutoka ndani ya pango ilikuwa vigumu kwa vile hapakuwa na sehemu ya kushika, pia giza la mle pangoni liliwafanya wasione njia ya kutokea.
Waliendelea kukumbatiana huku baridi la maji likizidi kuwapiga. Ng’wana Bupilipili alianza kutetemeka kwa meno kugongana.
SASA ENDELEA...
“Mume wangu nasikia baridi kali sana, pia nahisi mtoto atatuponyoka muda si mrefu, mikono imeishiwa nguvu kabisa.”
“Hataanguka mke wangu, nitamshikilia mpaka pumzi zangu za mwisho,” Mathayo alimpa moyo mkewe.
“Mume wangu bado siamini kama mtoto albino ni mkosi, kuna viumbe wangapi duniani ambao kwa akili ya kibinadamu tunawaona hawana thamani? Lakini kutokana na umuhimu wake wote Mungu amewathamini na kuwapa kipaumbele. Sasa itakuwaje kwa kiumbe huyu aliyepungukiwa na madini mwilini? Mwanangu na bundi nani mwenye thamani?”
“Mtoto.”
“Sasa mbona bundi hasakwi na kuuawa ila wanakimbilia kuua viumbe wasiyo na hatia. Hizo ni imani zisizo na ukweli zaidi ni kukubaliana na ujinga wa mtu mmoja na kuufanya ndiyo sheria.”
“Kwa kweli hata mimi bado sijaelewa hili suala la kuuawa albino ni nani aliyetoa wazo hilo.”
“Mume wangu unachekesha, yaani unachukua uamuzi wa kumuua mtoto wako kwa vile watu wamesema. Lakini hujui lolote kwa kile unachokifanya?” Ngw’ana Bupilipili alimshangaa mumewe.
“Mke wangu kwa hilo nakiri kosa, lakini nami naamini albino si mkosi.”
“Hivi mume wangu kama ningekukubalia tumtupe mtoto na baada ya siku ukayajua haya tunayozungumza, ungefanya nini?”
“Kweli ingeniuma, lakini ningekuwa nimefanya kosa la majuto.”
Mungu naye alishusha baraka zake, maji pangoni yalipungua kwa kasi, baada ya dakika ishirini maji yote yaliisha mle pangoni na kuweza kutoka salama na mtoto wao hadi juu ya pango.
Kila mmoja alikuwa akitetemeka kwa baridi kali, wingu bado lilikuwa limefunga na kufanya hali ionekane kama saa moja usiku na kumbe ni saa tano asubuhi. Walijiuliza watawezaje kurudi nyumbani kubadili nguo, kama kawaida mkewe pamoja na kuwa katika hali ngumu ya baridi, uchovu na njaa kali, aliamua kurudi kijijini na kumuachia mumewe mtoto ili akaandae chakula na kurudi na nguo za kubadili.
Aliendelea kumshukuru Mungu kwa kumlinda mtoto wao ambaye hakuguswa na maji. Kwa muujiza ule aliamini kabisa mtoto wao si mkosi kama walivyofikiria. Kwa mvua ile lazima kuna kitu kingetokea hata radi ambayo ingempiga na kumuulia mbali, lakini alibakia salama bila kupata madhara yoyote.
***
Alirudi hadi kijijini huku njia nzima ikiwa na vidimbwi vya maji. Kuna sehemu ilibidi avue nguo na kuziweka kichwani kutokana na mito kujaa maji na kufikia kifuani. Alitembea kwa shida bila kukutana na mtu. Alifika nyumbani na kuandaa chakula kingi ambacho wangekula kwa siku mbili. Baada ya kuandaa chakula, wakati wa kutoka alikutana uso kwa uso na jirani yake, mama Sabina.
“Jirani salama?”
“Salama.”
“Mvua imekuponesha?”
“Mmh! Namshukuru Mungu nimepita salama.”
“Mmh! Kuna usalama kweli?” Alimuuliza huku akimuangalia tumboni.
“Kwani vipi?”
“Mbona kama tumbo la mtu aliyejifungua?”
“Mama Monika, mbona maneno ya uchuro! Nijifungue kisha nikae kimya?” Ng’wana Bupilipili alipindisha ukweli.
“Aah! Basi macho yangu, kwani tumbo lako lilikuwa kubwa na sasa limepungua kidogo.”
“Bado mwezi mmoja.”
“Haya safari ya wapi tena na mvua hii?”
“Shamba.”
“Shamba wakati mvua ilikuwa ikitishia usalama?”
“Kuna sehemu ziliharibika mume wangu anazitengeneza hivyo nilikuwa nampelekea chakula.”
“Haya dada.”
Waliachana huku mama Monika akiwa haamini kabisa kauli ya Ng’wana Bupilipili juu ya kuwa na ujamzito. Wasiwasi wake huenda amejifungua njiti na mtoto akawa si riziki. Kwa hiyo aliona aibu kusema. Lakini kwa ujirani wao aliamini kama kumetokea tatizo lolote wasingemficha.
***
Kutokana na mawazo mengi, mama Sabina alimpita mumewe aliyekuwa akitoka ndani.
“Mama Sabina mbona hivyo?”
“Aah, kawaida tu mume wangu.”
“Halafu nimemuona mke wa Mathayo akielekea shamba, kuna nini wakati leo hali si nzuri, hata njia ya kuelekea shambani imejaa maji?” baba Sabina alimhoji mkewe.
“Unajua kuna kitu kinanichanganya.”
“Kitu gani tena mke wangu?”
“Unajua tokea jana asubuhi nilipokwenda kumjulia hali Ng’wana Bupilipili sikumkuta na baada ya muda nilimuona mume wake akiingia ndani majira ya alfajiri na baada ya muda alitoka na kikapu kilichoonekana kuna chakula.
“Siamini kama alifika mbali, baada ya kushika njia ya shamba tu mvua ilianza kunyesha. Lakini ajabu sasa hivi mke wake amerudi pia ameondoka na chakula na tumbo lake limepungua. Isijekuwa amejifungua mtoto ambaye hajatimia na kuamua kumzika ya bila kutushirikisha.”
“Sasa kwa nini wafanye hivyo?” baba Sabina aliuliza huku akiwasha gozo lake.
“Ndilo swali linaloniumiza akili.”
“Ulipomuuliza alisemaje?”
“Anasema yupo sawa, lakini kuna kitu ananificha...Halafu mimi nilifikiri kwa vile mvua imekatika kuna haja ya wao kurudi nyumbani. Nasikia mashamba mengi yamejaa maji sasa wao wanakwenda kufanya nini?”
“Mmh! Swali zito.”
“Lakini kuna kitu tutajua tu.”
“Mke wangu lisikuumize akili hilo, achana nalo.”
Mama Sabina alielekea jikoni kuandaa kifungua kinywa na kumwacha mumewe akilipuliza gozo
***
Baada ya mkewe kutoka, Mathayo alibakia na mtoto huku akiamini kabisa mvua ile ni mkosi wa kumficha mtoto albino ambaye alionekana ni mkosi. Wasiwasi wake mkubwa ulikuwa kwa wanakijiji kama wakijua ukweli.
Lazima hasira yao ingekuwa kubwa mara dufu hata kuwafanyia kitendo kibaya ikiwemo kuwaua kwa kuwafungia katika nyumba yao kwa muda mrefu ili wafe kwa njaa au kuwachoma moto wakiwa ndani.
Alijawa na mawazo mengi juu ya kuendelea kuwa na yule mtoto, bado aliamini ule ni mikosi na huenda ungewasababishia matatizo makubwa. Wazo alilokuwa nalo lilikuwa ni kukiulia mbali kile kitoto na kumweleza mkewe kuwa kilidondokea kwenye maji.
Lakini aliamini mkewe hawezi kumwamini hasa baada ya kutaka kumuua. Alijua chochote kibaya hata kama cha bahati mbaya kitaonekana cha makusudi.

Itaendelea
No comments: