Ismail Rage aikalia Yanga kooni

Baada ya kamati ya TFF ya katiba na sheria na hadhi za wachezaji kuitaka klabu ya Yanga kuilipa shilingi milioni 50 kama fidia kwa kitendo cha kumtumia beki Hassan Kessy wakati anamkataba na Simba, Ismail Rage amepinga hukumu hiyo.
rage-ismail
Mwenyekiti huyo wa zamani wa Simba ameitaka timu yake hiyo kutopokea kiasi hicho cha fedha kutoka kwa Yanga na badala yake waende mbele zaidi kupeleka malalamiko yao hayo kwa shirikisho la soka duniani Fifa.
“Maadam TFF wanakiri kwamba Kessy alikuwa mchezaji halali wa Simba SC na Yanga wamevunja mkataba kabla ya wakati, Yanga wanatakiwa wanyang’anywe pointi zote walizoshinda dhidi ya timu nyingine kabla ya uamuzi wa TFF,” amekiambia kipindi cha Sports Extra cha Clouds FM.
“Simba wanatakiwa wasichukue hizo milioni 50, watakuwa wamejidhalilisha sana. Kwa mujibu wa mkataba wa Simba, wanatakiwa wapate 1.2 billion kama dola 600,000 za kimarekani. Waende FIFA kwa ushahidi wote uliokuwepo na TFF wameshiriki kuvunja mkataba kwahiyo ushahidi upo wa kuwatia hatiani Yanga,” ameongeza.

No comments:

Powered by Blogger.