Serikali imedhamiria kukamilisha na kuimarisha mtandao wa usafirishaji na usambazaji umeme nchini ili kufikia malengo ya dira ya Taifa ya kufikia asilimia 75 ifikapo mwaka 2025 ya kuhakikisha miji na vijiji vyote Tanzania vinakuwa na umeme kila mahali.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa ameyasema hayo Jijini Dar es Salaam wakati akizindua mradi wa kuboresha upatikanaji wa umeme Jijini Dar es salaam, ambapo amesema kuwa hadi sasa serikali imeshatenga shilingi trilioni moja kwa ajili ya kusambaza umeme kwenye vijiji elfu nane nchi nzima ili wananchi wanaoishi maeneo hayo waweze kufanya shughuli zao za kiuchumi bila vikwazo.
Waziri Majaliwa ameongeza kuwa kwa kutambua tatizo la wananchi wasiokuwa na uwezo wa kulipia fedha nyingi za kuvuta umeme hasa wale wanaoishi maeneo ya vijijini, serikali kupitia shirika la umeme Tanzania-TANESCO imepunguza bei ya kuvuta umeme kwa wananchi hao ambapo wametakiwa kuvuta umeme huo kwa shilingi elfu ishirini na saba tu.
Awali akimkaribisha Waziri Mkuu kuzindua mradi huo, Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo amelitaka shirika la umeme TANESCO kuhakikisha tatizo la mgao na ukatikaji wa mara kwa mara wa umeme katika Jiji la Dar es salaam lisijitokeze tena.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Mhandisi Felchesmi Mramba amebainisha kuwa mradi uliozinduliwa leo umegharimu zaidi ya shilingi bilioni 70 ambapo mradi huo umelenga kutoa umeme wa uhakika kwa wananchi wote wa jiji hilo huku ukiwa na lengo la kutatua changamoto ya kulemewa kwa miundo mbinu ya umeme ambayo imekuwa ikizidiwa kutokana na ongezeko la mahitaji.
UNYAMA UNYAMA WAZIRI MKUU KASIM MAJALIWA AFANYA TUKIO ZITO USIKU HUU NEEMA YAANGUKA KWA WATANZANIA..
Reviewed by
Unknown
on
21:03
Rating:
5
No comments: