UJUMBE WA PLUIJM KWA MASHABIKI WA YANGA

Simba ikiwa katika msimamo mzuri katika ligi kuu katika nafasi ya kwanza, kocha wa Yanga amefunguka na kusema kwamba Simba lazima wakae chini.
Pluijm baada ya kupoteza mechi dhidi ya Mbeya City, Jumatano wiki hii kwa kufungwa mabao 2-1, amesema atahakikisha wanapata pointi tatu dhidi ya Prisons na kupunguza tofauti ya pointi kati yao na Simba.
“Mambo mengi yalitokea tukapoteza dhidi ya Mbeya City, lakini hiyo haiwezi kuwa maana ya kupoteza mechi zote za Mbeya, tuna mechi na Prisons naamini tutafanya vizuri baada ya maandalizi ya uhakika Tumebadilika kidogo hasa katika mbinu ili tuweze kupata pointi tatu ambazo zitapungua pointi kati yetu na timu inayoongoza, naamini itakuwa hivyo,” alisema Pluijm

No comments:

Powered by Blogger.