Huu Utajiri wa Donald Trump ni Kufuru Tupu....Angalia ushangae huyu jamaa alivyo balaah

DONALD TRUMP JOHN alizaliwa 14 Juni 1946 huko Jamaica Estates, Queens akiwa ni mtoto wa pipi kwenye familia ya watoto wanne wa familia ya Mary na Fred Trump na kukulia katika Jiji la New York, Marekani.

Upande wa baba yake (Fred Trump aliyefariki mwaka 1981), alikuwa mzaliwa wa Ujerumani na mama yake (Mary) ni mzaliwa wa Scottish.

Trump alianza kusoma katika Chuo Kikuu cha Fordham kilichopo Bronx mwaka 1964, miaka miwili baadaye alihamishiwa katika Shule ya mambo ya fedha na Uchumi ya Wharton iliyopo Chuo Kikuu cha Pennsylvania  ambako alihitimu shahada ya kwanza katika masuala ya uchumi mwaka 1968 kabla ya kujiunga na kufanya kazi kwenye kampuni ya familia yake iliyoitwa Elizabeth Trump & Son.

Mwaka 1971 Trump alikabidhiwa kuongoza makampuni na biashara za baba yake ambapo alipata mafanikio makubwa ndani ya muda mfupi ambayo mpaka sasa ndiye mkurugenzi wake mkuu.

Trump ambaye ni baba wa watoto watano, ni mfanyabiashara mkubwa na bilionea nchini Marekani, pia ni mtayarishaji wa vipindi vya televisheni.

Baadhi ya mali anazomiliki

Trump Ocean Club International Hotel and Tower lililopo Panama City, Panama

Trump Tower lililopo Manhattan

Wollman Rink lililoko Central Park

Trump Taj Mahal lililoko Atlantic City, New Jersey

Turnberry Hotel, iliyoko Ayrshire, Scotland

Trump Hotel Las Vegas

Trump International Hotel & Tower ya New York

Trump International Hotel & Tower ya Chicago

Trump International Hotel ya Las Vegas

Trump International Hotel ya Waikiki Beach Walk

 Trump SoHo ya New York

Trump International Hotel & Tower ya Toronto

Taasisi ya Donald J. Trump

Branding na licensing

Ndege kubwa ya Trump’s Boeing 757, maarufu kama “Trump Force One”.

Utajiri

Mwaka huu (2016), Jarida maarufu la Forbes lilikadiria utajiri wa mali za Trump kuwa unafikia dola bilioni 3.7. Ameweka rekodi ya kuwa mwanasiasa mwenye utajiri mkubwa zaidi kwenye historia ya nchi hiyo.

Ikijumulishwa na thamani ya kampuni yake (brand), Trump anakadiliwa kuwa na utajiri sasa wa dola bilioni 10 na kuwa tajiri namba 324 wa dunia na wa 156 kwa nchi ya Marekani.

Trump ni Mwenyekiti na Rais wa Shirika Kibiashara la Trump (Trump Organization) lenye makao yake makuu katikati ya Mji wa Manhattan ambalo linamiliki majengo mengi marefu, hoteli, kasino,  timu za gofu, ndege na miradi mbalimbali mikubwa ya maendeleo nchini Marekani na nje ya Marekani.

Ni mwanasiasa wa Chama cha Republican na anagombea urais wa Marekani kupitia chama hicho mwaka huu, uchaguzi utaofanyika Novemba 8. 

No comments:

Powered by Blogger.