HABARI NZITO YA HIVI PUNDE: JESHI LA POLISI LAFUNGUKA MAZITO JUU YA TUHUMA NZITO ZA RUSHWA KWA KAMANDA SIRRO..

MAKAO Makuu ya Jeshi la Polisi nchini imesema inachunguza tuhuma zilizotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda dhidi ya Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna wa Polisi Simon Sirro na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Kamishna Msaidizi Suzan Kaganda kuhongwa ili wasidhibiti matumizi ya dawa za kulevya aina ya shisha.

Makonda alitoa tuhuma hizo baada ya kudai kuwa viongozi hao wa polisi wamekuwa wakilegalega kusimamia ipasavyo kukomesha matumizi ya dawa za kulevya, aina ya shisha.Kaimu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai katika makao makuu ya jeshi hilo, Kamishna wa Polisi, Robert Boaz alisema hayo jana wakati akijibu swali kuhusu hatua za jeshi hilo zilizochukuliwa kutokana na tuhuma zilizotolewa na Makonda. “..kama ilivyo taratibu zetu tunapopokea tuhuma dhidi ya kiongozi wa jeshi hili au askari yeyote tunafanya uchunguzi, kwa hiyo hata tuhuma hizi tunazifanyia uchunguzi kubaini kama ni kweli,” alisema alisema Boaz.

Wiki hii wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Uboreshaji wa Miundombinu ya Umeme katika Jiji la Dar es Salaam uliofanywa na Waziri Mkuu, Makonda aliwatuhumu viongozi hao wa polisi kwa kulegalega kusimamia suala hilo huku akihofia wanaweza kuwa wamehongwa na watu waliotaka kumhonga yeye lakini akakataa.

Lakini mkuu huyo wa mkoa alienda mbali zaidi na kudai kuna kikundi cha watu 10 waliokwenda kwake ambao anawatambua kama “maajenti wa shetani” ambao wanapata faida kati ya Sh milioni 35 mpaka Sh milioni 45 kwa mwezi kutokana na dawa hizo za kulevya.

No comments:

Powered by Blogger.