Utani wa Zitto Kabwe kwa Mbowe kushangilia goli la mkono la Tambwe

Timu za Simba na Yanga mara nyingi zinapokutana huwa kuna mambo mengi ya kuchekesha huwa yanajitokeza, hususani utani wa mashabiki wa pande zote mbili kutoleana maneno ya utani kabla na baada ya mechi, hususani timu moja wapo inapomfung mwenzake.

October 1 2016 uwanja wa Taifa Dar es Salaam katika mchezo wa watani wa jadi uliochezwa na kumalizika kwa sare ya goli 1-1, Freeman Mbowe  ambaye ni mbunge na kiongozi wa chama cha siasa cha CHADEMA alikuwa ni moja kati ya mashabiki wa Yanga waliojitokeza na kushangilia kwa furaha goli la Amissi Tambwe lililofungwa mkono ukiwa umehusika kucheza mpira.

Zitto Kabwe

Baada ya mechi mbunge wa Kigoma mjiniZitto Kabwe ambaye ni shabiki wa Simbaalitumia account yake rasmi ya twitter na kuandika ujumbe wa utani kwa Freeman Mbowe ambaye alishangilia goli la utata la Tambwe “Mwenyekitiwangu Freeman Aikaeli Mbowe anatambua goli la mkono la Tambwe lakini hamtambui Lipumba “

No comments:

Powered by Blogger.