inasikitisha kijana atobolewa macho na kibaka mchana kweupe

September 29, 2016 kijana mmoja kutoka Mabibo Hostel jijini Dar es salaam alitobolewa Macho na mtu aliyefahamika kwa jina la Scorpion ambaye kwa mujibu wa maelezo ya kijana huyo ilidaiwa kuwa anaogopwa sana kutokana na historia ya matukio aliyokuwa akiyafanya mara kwa mara.

Leo September 30, 2016 darubiniyako imefuatilia mkasa huo kiundani zaidi kwa wananchi wa eneo hilo na wengine kukiri kushuhudia tukio alilofanyiwa kijana huyo lakini walishindwa kutoa msaada kwasababu tu Scorpion alikuwa na uwezo wa kumdhuru mtu na hatua zisichukuliwe juu yake. 

>>>’Watu wote wanamuogopa hawakuthubutu kusogea wala kumtetea inasemekana hili ni tukio lake la tatu…… ila sisi tuna hofu hatuna amani yule akikutamani umekishwa kwa sababu yeye anavyokufuata watu wote watabaki kuangalia tu huna mtetezi mpaka jama atakapo jiridhisha:–Mkazi Buguruni

>>>Ni kweli hilo tukio limetokea na polisi tayari walishachukua hatua kwa maana ya huyo mtuhumiwa Scorpion jina lake halisi anaitwa Salum Mpepe alikamatwa siku ya tarehe 12 mwezi wa 9 akawa pale kituo cha polisi Buguruni wakati upelelezi ukiendelea tarehe 23 mwezi wa 9 alifikishwa mahakami na kusomewa jinai namba 276 unyang’anyi kwa kutumia silaha, yupo magereza kesi yake itatajwa tena tarehe 5 mwezi wa 10 2016:- 

No comments:

Powered by Blogger.