SIMBA Vs Yanga: Mabomu ya machozi yalindima Uwanjani

Mashabiki wa Simba uzalendo uliwashinda baada ya bao la Amissi Tambwe na kumua kurusha viti uwanjani wakipinga bao hilo, kutokana na kitendo hicho askari wa kutuliza ghasia waliamua kurusha mabomu ya machozi jukwaani.

Mabomu hayo ya machozi yaliwafanya mashabiki wa Simba waliofurika uwanjani hapo kuanza kukimbia hovyo kujinusuru na mabomu hayo huku wengine wakitoka nje kabisa ya uwanja. Mashabiki baadhi wameumia kutokana na vurugu hizo.

Kutokana na vurugu hizo mchezo huo ulisimama kwa dakika kadhaa kabla ya mwamuzi Martin Saanya kutoa kadi nyekundu kwa nahodha wa Simba, Jonas Mkude.

Awali baada ya bao la Yanga, mzee mmoja shabiki wa Simba aliyevalia jezi nyekundu alitaka kuingia katika vyumba vya kubadilishia nguo vya Yanga. Kitendo hicho kiliwaudhi makomandoo wa Yanga ambao walimkamata na kuanza kumpiga kabla ya askari wa kutuliza ghasia kuingilia kati kumnusuru na kipigo hicho.

Kabla ya mechi kuanza Mzee huyo alikuwa amekaa katika mlango wa kuingilia vyumba vya kubadilishia nguo wachezaji wa Simba.

No comments:

Powered by Blogger.