Jinsi Simba walivyo badili upepo #SimbaVsYanga

Mshambuliaji wa Yanga, Amis Tambwe akimtoka beki wa Simba, Novaty Lufunga katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. (Picha na Francis Dande)

 Wachezaji wa Yanga wakishangilia bao lililofungwa na Amis Tambwe.

 Furaha ya ushindi.

 Wachezaji wa Simba wakimlalamikia mwamuzi Martin Saanya.

 Mzozo.

 Wakialalamika

 Wachezaji wa Simba wakimzonga mwamuzi.

 Amis Tambwe akiwa na kocha wake.

 Jonas Mkude akitoka nje baada ya kuonyeshwa kadi nyekundu.

 Mkude akitoka nje.

 Shabiki akikimbizwa kup[ata huduma ya kwanza baada ya kuumia kichwani.

 Ibrahim Ajibu akimtuliza Martin Saanya.

 Mashabiki waliokuwa jukwaa la Simba wakikimbia baada ya Polisi kupiga mabomu ya machozi.

WATANI wa jadi, Simba na Yanga wamegawana pointi baada ya kutoa sare ya kufungana bao 1-1 katika mchezo wa Ligi Kuu yaTanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Ushindi unazidi kupandisha kileleni Simba SC ikifikisha pointi 17, baada ya kucheza mechi saba, wakati Yanga inatimiza pointi 11 baada ya kucheza mechi sita.
Katika mchezo wa leo Yanga mabingwa wa ligi hiyo walitangulia kwa bao la mchezaji hatari, Amissi Joselyn Tambwe kabla ya  Shizza Ramadhani Kichuya kuisawazishia wazee wa msimbazi, Simba SC iliyocheza pungufu  baada ya Jonas Mkude kutolewa kwa kadi nyekundu kwa kosa la kuongoza fujo na kumtukana refa kipindi cha kwanza.Tambwe alifunga bao lake dakika ya 26, akimalizia pasi ndefu ya beki Mbuyu Twite na kugeuka mbele ya beki wa Simba, Novat Lufunga kabla ya kufumua shuti lililomshinda kipa Vincent Angban wa Simba .
Bao hilo lilizua kizaazaa, wachezaji wa Simba wakimvaa refa Martin Saanya wakidai mfungaji, Tambwe aliushika mpira kabla ya kufunga, shutuma ambazo si za kweli
Katika vurugu hizo, Saanya akamtoa kwa kadi nyekundu Nahodha wa Simba SC, Jonas Mkude dakika ya 29 kwa sababu ndiye aliyekuwa mstari wa mbele, kutukana na kufanya fujo. Pia mchezo ukasimama kwa takriban dakika tano baada ya mashabiki wasio na nidhamu wa Simba kuanza kufanya vurugu waking’oa viti na kutupa uwanjani.
Polisi walitumia milipuko kuwatuliza mashabiki hao na mchezo ukaendelea.
Kipindi cha pili, Simba SC walibadlika pamoja na kucheza nguvu wakafanikiwa kupata bao la kusawazisha lililofungwa na winga Shizza Kichuyaa dakika ya 87 baada ya kona aliyochonga kuingia moja kwa moja nyavuni. Hadi mwisho wa mpambano Bebi Salome Simba 1 na dume la nyani Yanga  1
Kikosi cha Yanga SC kilikuwa; Ally Mustafa 'Barthez',Juma Abdul,Mwinyi Hajji, Kevin Yondan/Andrew Vincent dk46, Vincent Bossou, Mbuyu Twite, Juma Mahadhi/Simon Msuva, Thabani Kamusoko, Amisi Tambwe, Donald Ngoma na Deus Kaseke/Haruna Niyonzima.

Simba SC; Vincent Angban, Janvier Besala Bokungu, Mohammed Hussein 'Tshabalala', Novart Lufunga/Juuko, Method Mwanjali, Jonas Mkude, Shizza Kichuya, Muzamil Yassim, Laudit Mavugo/Blagnon, Ibrahim Hajib/Mohamed ‘Mo’ Ibrahim na Mwinyi Kazimoto.

No comments:

Powered by Blogger.