SIRI Zaidi Zavuja Kiburi cha Prof Lipumba CUF Hiki Hapa

Kile kinachoonekana kumpa nguvu ya kuendelea kuwa mwenyekiti wa CUF licha ya songongombingo zinazoendeshwa dhidi yake ni kutokufuatwa kwa katiba ya chama hicho utafiti wa Jamvi la Habari umebaini.

pamoja na kutokufuatwa kwa ibara ya 171 ya chama hicho inayomuhitaji kiongozi kukubaliwa kujiuzulu kwake na mkutano ama kikao kilichomchagua, lakini pia ibara ya 77 (7) ya chama hicho inambeba zaidi na kuwanyima utetezi upande unaompinga.

Soma mwenyewe hapa.

Ibara 77 (7)

NUKUU :
Maamuzi muhimu yatahesabiwa kuwa maamuzi halali ya Mkutano mkuu wa Taifa ikiwa zaidi ya theluthi mbili (2/3) ya wajumbe kutoka Tanzania Bara waliohudhuria. Na zaidi ya theluthi mbili (2/3) ya wajumbe kutoka Zanzibar waliohudhuria watayaunga mkono maamuzi hayo.
Ibara ya 77 (8)
NUKUU :
Kwa madhumuni ya Kifungu cha (7) cha Kifungu hiki maamuzi muhimu ni pamoja na :-
(a) Kuvunja Chama.
(b) Kubadilisha Jina la Chama.
(c) Kuunganisha Chama na Chama au vyama vya Siasa vingine.
(d) Kuwasimamisha , Kuwaachisha au Kuwafukuza uongozi na / au uwanachama viongozi wakuu wa kitaifa wa chama pamoja na viongozi wa kitaifa kama ilivyoainishwa ndani ya katiba hii.
(d) Kuwaachisha , Kuwafukuza uwanachama Rais na /au Makamu Rais wa Jamuhuri ya Muungano na Rais wa Zanzibar anayetokana na Chama.
(f) Kupitisha , Kurekebisha au Kubadilisha katiba hii au Kifungu chochote cha katiba hii.
(g) Kupitisha , Kurekebisha au Kubadilisha itikadi ya Chama.
(h) Mambo mengine yoyote ambayo Mkutano Mkuu wa Taifa kwa masharti yale yale ya Kifungu cha (7) cha kifungu hiki utaamuwa kuwa ni maamuzi muhimu.

No comments:

Powered by Blogger.