BUNGE Kufikishwa TAKUKURU Kwa Tuhuma za Rushwa

Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA), inakusudia kuzifikisha taasisi tisa za serikali katika Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, (TAKUKURU) ili kuchunguzwa kutokana na kuonesha viashiria vya rushwa.

Taasisi hizo ni Ofisi ya Bunge, Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, TCRA, DART, Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma pamoja na Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge. Nyingine ni Wakala wa Umeme Vijijini (REA), na Makumbusho ya Taifa ambazo zina viashiria uwezekano wa kuwepo kwa vitendo vya rushwa.

Mwenyekiti wa Bodi ya PPRA, Balozi Dk. Marten Lumbanga, amesema hayo leo Jijini Dar es Salaam wakati akiongea na vyombo vya habari, na kueleza kuwa katika ufuatiliaji wa tuhuma 14 ndani ya taasisi nyingine 8 wamebaini serikali imepata hasara ya shilingi bilioni 23.41 kutokana na ukiukwaji wa sheria na taratibu za manunuzi kwa mwaka wa fedha 2015/2016.

Balozi Lumbanga amesema Jumla ya Mikataba 21,313 ya manunuzi yenye thamani ya shilingi trilioni 1.5 imefanyiwa ukaguzi, ambapo PPRA itachukua za kinidhamu kwa watumishi waliohusika katika miradi 15 iliyopata alama mbaya katika kupima thamani halisi ya malipo, na kuwataka wakuu wa taasisi zenye malipo yenye utata kurejesha fedha ndani ya miezi mitatu.

No comments:

Powered by Blogger.