Profesa Tibaijuka akataa zaidi ya Sh 200 milioni za tuzo
Mbunge wa Muleba Kusini, Profesa Anne Tibaijuka.
Dar es Salaam. Mbunge wa Muleba Kusini, Profesa Anne Tibaijuka amesema amepata tuzo nchini Marekani ikiwa ni kuthamini mchango wake akiwa Umoja wa Mataifa lakini akakataa kuchukua fedha dola 100,000( zaidi ya Sh 200 milioni) ambazo huambatana na tuzo hiyo.
Alisema alikataa kupokea fedha hizo kwa sababu maadili ya nchi yetu hayaruhusu kupokea zawadi kama hiyo.
Alisema lakini aliwaeleza kwamba katika mkoa anakotoka kumetokea tetemeko la ardhi na kuna maafa.
Alisema wao wataamua cha kufanya lakini yeye binafsi amekataa kupokea fedha hizo.
No comments: