MIKAKATI YA YANGA OCT 1,HII HAPA SIMBA ACHOMOKI
Kikosi cha yanga ambacho jana Septemba 25 kilishtukizwa kwa kichapo cha kwanza katika ligi kuu ya soka ya Vodacom baada ya kukubali kichapo cha bao moja kwa bila kutoka Stand United ya Shinyanga kinakabiliwa na mchezo mgumu wa ligi hiyo dhidi ya Simba Octoba 1, mwaka huu.
Tumetaka kujua Yanga watakita wapi kambi yao kujiwinda na mahasimu wao hao wa jadi katika soka la Tanzania, ndipo tulipokutana na sentensi za Katibu Mkuu wa Wanajangwani hao kama ifuatavyo...
>>>Kikosi chetu kitaendelea kuweka kambi mkoani Shinyanga au kitakwenda Mwanza kwa ajili ya kujiandaa na mechi yetu dhidi ya Simba ambapo kitarejea siku chache kabla ya mchezo.
>>>Mchezo wa Simba ni wa kawaida kwetu na tunajiandaa kama ilivyo kwa mechi nyingine kwani tumeshakutana na timu kubwa ikiwemo TP Mazembe, hivyo tunaupa uzito sawa mchezo huo na ile mingine.
Pamoja na sentensi hizo, usione ajabu kama Yanga wataamua kubadili upepo kwa sababu michezo inayowahusisha watani wa jadi hao hugubikwa na maandalizi mengi yenye usiri na maamuzi ya ghafla.
No comments: