Mch. Msigwa aibomoa TCRA, aibeba ITV
Niliwahi kusema Bungeni Kuwa tumezalisha taifa la watu wanafiki waoga na kujipendekeza pendekeza, ITV KOSA LAO NINI? Mimi ndiye nilikuwa naongea , aliyekuwa ananihoji angejuaje nakwenda kuongea nini? Kwa nini hiyo adhabu wasinipe mimi?aliyekashifiwa kwa mujibu wa TCRA ni Ndugu Tulia , yeye ndiye alipaswa kunipeleka mahakamani kama anahisi kukashifiwa. Naiona hii ni njama ya kutisha vyombo vya habari visiwe vinatualika kwenye mahojiano kwenye vipindi vyao. Watu wamejaa HOFU, uoga, mashaka na kutojiamini, maisha ya kujipendekeza ni magumu mno ,
Tafsri nyepesi ya maisha ya kujipendekeza nikuamini kuwa mtu mwingine anazofunguo za mafanikio yako yaani bila yeye hutaweza, hivyo inakulazimu kuishi kwa kutekeleza ndoto zake.
No comments: