Picha ya Yesu Akitokwa Damu Msalabani Yaonekana Kanisani Nigeria
Picha ya Yesu msalabani inayodaiwa kutokwa damu.
Mwanga mkali kanisani baada ya picha ya Yesu kudaiwa kuonekana.
Kanisa Katoliki la Mtakatifu Agustino ambapo muujiza huo unadaiwa kutokea.
Waumini wakiwa wamekusanyika eneo la picha ya Yesu msalabani iliyokuwa ikitokwa damu.
Maelfu ya wakazi wa Jimbo la Benue nchini Nigeria, wakristu na wasio wakristu jana walifurika katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Agustino lililopo karibu na Mji wa Makurdi kushuhudia muujiza wa kuonekana kwa picha ya Yesu msalaani ikitoka damu.
Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo wanasema waliona picha ya Yesu katika ukuta ndani ya kanisa hilo wakati mashuhuda wengine wakisema waliona picha ya Yesu msalabani ikitokwa damu ambayo ilikuwa ikichuruzika kuelekea miguuni.
Mmoja wa waumini wa kanisa hilo alisema picha ya kwanza ilitokea Ijumaa iliyopita na baada ya taarifa kusambaa sana siku ya Jumapili, kesho yake Jumatatu (juzi) wananchi wakakimbilia kanisani hapo kushuhudia miujiza hiyo.
Mmoja wa waumini aitwaye, Emmanuel Hembenkaan alisema picha iliyoonekana ukutani iliambatana na mwanga mkali ambao uliangaza ndani ya kanisa zima.
Chanzo: NaijaGists.com
No comments: