BILIONEA WA CHADEMA AIKANA CCM KUHUSU DODOMA
Mfanyabiashara maarufu nchini, Mustafa Sabodo ameitaka Serikali kuwachangisha wananchi ili kupata fedha za kuhamishia makao makuu ya Serikali mjini Dodoma.
Sabodo ambaye hivi karibuni alisema kuwa amesitisha misaada yake kwa CHADEMA na kuhaidi kuwa atachangia trilioni 10 za kuisaidia Serikali kuhamia Dodoma amesema kua hana pesa hizo.
Akizungumza jana katika mahojiano maalumu nyumbani kwake Upanga jijini Dar es Salaam, Sabodo alisema hana fedha za kutoa kwa ajili ya maandalizi ya ujenzi wa miundombinu mkoni Dodoma.
“Nataka niweke suala hili vizuri, sina fedha za aina hiyo popote pale. Ninazo mali kadhaa lakini sina fedha zote hizo. Watu wengi wanakuja kwangu, wanakuja hapa, nipe pesa, nipe pesa, hakuna pesa hapa,” alisema Sabodo na kuongeza:
“Mimi ni kama kichocheo tu, kama ndimu unatia kwenye soda. Nilichosema ni kutafuta juhudi kutoka kwa kampuni za India na Singapore kufanikisha ujenzi wa makao makuu ya Dodoma, lakini sina kiasi chote hicho cha fedha,” alisema.
No comments: