WAKATI MO AKIJADILIWA ,BAKHRESA AJITOKEZA NA BILIONI 40 ZA KUITAKA SIMBA,AVEVA ANENA HAYA

WAKATI wanachama wa Klabu ya Simba wakiwa katika mchakato wa kujadili mabadiliko ya uendeshwaji wa klabu hiyo kwa kuuza hisa ili kujitegemea kiuchumi, Kamati ya utendaji ya klabu hiyo imekutana leo kupitisha agenda zitakazojadiliwa kwenye mkutano mkuu utakaofanyika Jumapili, Dar es Salaam
Awali, suala la udhamini lilianzia kwa bilionea Mohammed Dewji 'Mo', sasa linaonekana kuchukua sura nyingine baada ya kudaiwa mfanyabiashara mwingine Said Salim Bakhresa (SSB), kupitia kampuni yake ya Azam Media naye kuwa tayari kuwekeza kwenye klabu hiyo.

Taarifa ambazo zimepatikana , zinadai kuwa imeundwa kamati maaulum inayojulikana kwa jina la 'SSI' inayoratibu mchakato huo wa kusaka wadhamini, na endapo mipango itakwenda vizuri, SSB wanatarajiwa kutoa udhamini wenye thamani ya Sh. bilioni 40 katika kipindi cha miaka mitano, ikiwamo kusaidia ujenzi wa uwanja.

 Rais wa Simba, Evans Aveva alisema kikao hicho kitatoa mwelekeo wa kila kitakachojadiliwa katika mkutano wa wanachama.

Aveva alisema kuwa suala la kumuuzia hisa bilionea Mo 'joto' lake liko juu na kupitia mikutano mbalimbali ya matawi inayofanyika, viongozi wanapokea maoni ili kujua kile ambacho wanachama wanahitaji.

"Suala la Mo niseme wazi kuwa bado lipo kwenye mapambano na mbio zake zinaonyesha ni mtu mwenye nia ya kweli ya kununua hisa, ila mwisho wa siku wenye timu wataamua," alisema Aveva.

Kuhusiana na suala la Azam Media, Aveva alikanusha kuwepo kwa mazungumzo ya kutaka kununua hisa, lakini akaeleza kwamba wamefanya mazungumzo na kampuni hiyo kwa ajili ya kudhamini Tamasha la Simba Day Agosti 8 jijini

No comments:

Powered by Blogger.