Kuporomoka Kwa Akiba ya Fedha za kigeni Tanzania nani alaumiwe??

::USD 500m zimepungua kwenye Foreign Reserve. Kuna ' jambo ' kubwa kwenye Akiba ya Fedha za Kigeni Tanzania::

Nikiwa nasoma Taarifa ya IMF ( IMF Executive Board Completes Fourth PSI for Tanzania and Concludes 2016 Article IV Consultation) kuhusu Tanzania niliona kuwa Akiba yetu ya Fedha za kigeni imeshuka ' Akiba ya kuweza kuhudumia miezi 4.1 ya bidhaa tunazoagiza kutoka nje. Taarifa hii http://www.imf.org/external/pubs/ft/scr/2016/cr16253.pdf inaonyesha kuwa Akiba ya Fedha za kigeni ya Tanzania imeporomoka mpaka ' Akiba ya kuweza kuhudumia miezi 3.6 ya bidhaa tunazoagiza kutoka Nje'. Sikuamini ikabidi nikatazame Taarifa za Benki Kuu.

Taarifa ya Benki Kuu ya Mwezi Novemba ( BOT Monthly Economic Review ) inaonyesha kuwa Tanzania ilikuwa na Akiba ya USD 4bn ambayo inatosha kuagiza bidhaa kwa miezi 4. Hata hivyo BOT wanaonyesha kuwa ilipofika mwezi April 2016 Akiba ya Fedha za kigeni ilishuka mpaka USD 3.8bn na Mwezi Juni imeshuka mpaka USD 3.5bn.

Katika kipindi ambacho bei ya mafuta bado ipo chini na mauzo nje bado hayajashuka ilitakiwa Foreign Reserve yetu iongezeke sio kupungua.

Kuna jambo kubwa linaendelea kwenye Akiba ya Fedha za kigeni ya Tanzania. Ama Serikali kupitia Benki Kuu inapunguza Akiba ili kuibeba Shilingi isishuke thamani au Akiba imetumika kwa matumizi ya kawaida. Serikali haina budi kutoa maelezo ya kina.
http://www.imf.org/external/pubs/ft/scr/2016/cr16253.pdf
By
Zitto Kabwe
Source FB

No comments:

Powered by Blogger.