YANGA KUTIMKIA UTURUKI JUMAPILI.
MABINGWA wa ligi kuu Vodacom 2015/2016 Yanga wanatarajia kuondoka siku ya jumapili Juni 12 kuelekea nchini Uturuki kwa ajili ya kuweka kambi kujiandaa
na mchezo wa hatua ya robo fainali ya Kombe la shirikisho dhidi ya Mo Bejala utakaopigwa Juni 19 nchini Algeria.
Yanga itaweka kambi nchini Uturuki na itakaa kwa siku chache kabla ya kuunganisha moja kwa moja nchini Algeria kwa ajili ya mchezo wa kwanza na Mo bejan ya Algeria kati ya tarehe 17,18,19 mwezi huu.
Akitoa taarifa hiyo, Mkuu wa kitengo cha habari na Mawasiliano Jerry Muro amesema kuwa kikosi kitaondoka mapema na kuweka kambi Uturuki ikiwa ni moja ya mikakati ya mwalimu Hans Van De Pluijm katika kujiandaa na mchezo huo wa kwanza na pia kuwajenga kisaikolojia wachezaji hususani kutokana na mechi za ugenini kuwa ngumu sana na fitina pia.
"Timu itaondoka jumapili kuelekea Uturuki na lengo kuu sana ni kuweza kukiandaa kikosi vizuri kuelekea mchezo wetu dhidi ya Mo bejala na tunafahamu utakuwa ni moja ga mechi ngumu sana kwanj tunafahamu tutakuwa ugenini na watatumia mbinu mbalimbali za kututoa mchezoni lakini tunajua jinsi ya kupambana nazo kwahiyo wachezaji watajengwa kisaikolojia na kuweza kutoka na ushindi,"amesema Jerry.
Yanga itaondoka na wachezaji 20 huku Juma Abdul akisalia nchini kutokana na kuwa majeruhi akiumia kifundo cha mguu na nafasi yake kuchukuliwa na Hassan Kessy
No comments: